Wednesday, 18 November 2015

Uteuzi wa Waziri Mkuu: Spika Job Ndugai Kukabidhiwa Bahasha ya Jina La Waziri Mkuu Kesho.....Ijumaa Kuapishwa

 
Baada ya wabunge kumchagua Mbunge wa Kongwa, Job Ndugai kuwa Spika wa Bunge la 11 jana, anayesubiriwa ni Waziri Mkuu mpya ambaye anatarajiwa kujulikana kesho

Kwa mujibu wa ratiba ya vikao vya Bunge, kesho Alhamisi, Bunge litapokea na kuthibitisha kwa kupiga kura jina la Waziri Mkuu wa 11 wa Tanzania ambalo Dk Magufuli atakuwa ameliwasilisha kwa Spika Job Ndugai.

Baada ya kutoa  jina la Waziri Mkuu, Dk Magufuli anatarajia kulihutubia Bunge, Ijumaa saa kumi baada ya kuwa amemwapisha Waziri Mkuu asubuhi.

Hotuba yake ya Kwanza Bungeni  itakuwa dira ya utawala wake kwa miaka mitano ijayo akiwa na kauli Mbiu ya Hapa kazi tu

0 comments: