Watu watatu wamefikishwa Mahakama ya Mkoa wa Mwanza wakikabiliwa na mashtaka ya wizi wa kimtandao na kujipatia Sh4 milioni kwa njia ya udanganyifu.
Washtakiwa hao wanadaiwa kusajili namba za simu za uongo, huku wakifungua akaunti ya benki ya NMB kwa jina la vyama vya Chadema na CCM wakitaka wachangiwe fedha za kuendesha kampeni za Uchaguzi Mkuu
Wakili wa Serikali, Castuce Ndamugoba aliwataja washtakiwa hao kuwa ni Bony Tefe (40), mkazi wa Mahina, Spridon Njunwa (38) mkazi wa Igoma, na Briton Wilson (43) ambaye ni fundi cherehani na mkazi wa Bugando, Mwanza
0 comments:
Post a Comment