Polisi wametoa picha ya raia wa Ufaransa anayetafutwa akihusishwa na mashambulio ya jijini Paris yaliyoua watu 129.
Mtu huyo ajulikanaye kwa jina la Salah Abdeslam, mwenye miaka 26, anaelezwa kuwa mtu hatari.
Ripoti zinasema ametambuliwa kuwa alikodi gari lililotumika kwenye shambulio wakati yeye na watu wengine wawili waliposimamishwa na polisi karibu na mpaka wa Ubelgiji.
Imeelezwa kuwa maafisa walimruhusu kuendelea na safari yake baada ya kutazama kitambulisho chake.
Katika hatua nyingine, ndege za kivita za Ufaransa zimetekeleza mashambulizi katika mji wa Raqqa nchini Syria, ngome ya wanamgambo wa Islamic State.
Operesheni hiyo imekuja siku mbili baada ya mashambulizi ya jijini Paris,ambayo wanamgambo wa Islamic state wamekiri kuhusika.
Ndege 12 za kijeshi za Ufaransa zimedondosha mabomu 20.
Wizara ya ulinzi imesema maeneo kadhaa yamelengwa yakiwemo maeneo yaliyo na silaha za wanamgambo na kambi za mafunzo za wapiganaji hao.
0 comments:
Post a Comment