Saturday, 21 November 2015

Kauli ya Zitto Kabwe Kuhusu Wabunge wa UKAWA Kuitwa "Watoto" Bungeni

 

WAKATI Rais Magufuli akimpa heko Mbunge wa Kigoma Mjini Kupitia chama cha ACT Wazalendo Zitto Zuberi Kabwe kwa kitendo chake cha kutoungana na wabunge wanaowakilisha umoja wa katiba ya wananchi Ukawa kupiga kelele na kutolewa nnje ya Bunge na Spika Job Ndugai,Zitto ameibuka na kuwaunga mkono wabunge hao.

Akizungumza nje ya bunge, muda mfupi mara baada ya bunge hilo kuhairishwa na Waziri Mkuu Mhe Kasimu Majaliwa,Zitto alisema kuwa hakuna haja ya kuwajadili wabunge hao kwa kuwa demokrasia inawapa haki ya kufanya hivyo.

Zitto ambaye alikuwa akizungumza na Shirika la Habari Tanzania’TBC’ alisema kuwa haoni sababua ya wabunge hao kuitwa wahuni au watoto kama walivyoitwa Bungeni kwa kuwa kufanya hivyo ilikuwa ni sehemu ya kuwasilisha hisia zao kwa walengwa.

Alisema kuwa binafsi hana muda wa kulijadili suala hilo kwa kuwa limeshapita na kinachotakiwa kwa sasa ni kufanya kazi iliyowapeleka bungeni.

0 comments: