Sunday, 15 November 2015

Mkwasa Afunguka: Tulifanya Kosa Kubwa Sana Kufanya Mabadiliko ..

Baada ya timu ya taifa ya Tanzania ‘Taifa Star’ kulazimishwa sare ya kufungana magoli 2-2 na Algeria kwenye uwanja wa taifa, kocha mkuu wa kikosi hicho Charles Boniface Mkwasa amesema, mabadiliko yaliyofanywa na benchi la ufundi kumtoa Elius Maguli na kumingiza Mrisho Ngassa hayakuzaa matunda kama walivyotarajia.

Mkwasa amesema, walimuanziasha Maguli kwasababu ni mchezaji ambaye anatumia nguvu na anaweza kupambana kwa kutumia mwili wake lakini baadaye walimpumzisha wakiamini kuingia kwa Ngassa kungeifanya timu kutengeneza  nafasi nyingi zaidi za kufunga kwasanbabu Ngassa anaspidi na uwezo wa kutengeneza nafasi.

“Niseme tu kwamba leo (jana) ilikuwa ni game yetu 100%  tumetengeneza nafasi nyingi sana lakini tumeshindwa kuzitumia tumepata goli mbili lakini kuna muda tumepoteza concentration wakaweza kurudisha goli zote mbili lakini vijana wamepambana wamehangaika kutafuta magoli kutokana na nafaisi zilizopatikana na wakati mwingine tunasema mpira unabahati na Algeria wanabahati sana”, alisema Mkwasa.

“Vijana wamejitahidi lakini niseme tulifanya makosa pengine wakati wa kufanya mabadiliko kwasababu timu ilishakuwa stable lakini ni matokeo ya mchezo na nafikiri bado tunamlima mrefu kwasababu ninavyowatazama hawa nyumbani kwao watabadilika. Lakini uwezo wa kuwafunga tunao timu yao sio nzuri sana kiasi kwamba haifungiki”.

“Niwashukuru watanzania na waandishi wa habari kwa kuhamasisha na watanzania wameweza kuitikia na tumeona jinsi gani wameishangilia timu yao lakini wasife moyo kwa matokeo haya, tupo katika mchakato wa kujenga timu naamini katika muda mfupi tutakuwa na timu nzuri kama wenzetu ambavyo wanatimu zao”.

“Niwashukuru pia wachezaji na wengine wote ambao tumeshirikiana, kamati pamoja na TFF kwa kuweza kuonesha kiwango ambacho kwa muda mrefu hakijaonekana”.

Kikosi cha Stars kimeondoka jana usiku kuelekea nchini Algeria kwa ajili ya mchezo wa marudiano utakaopigwa Jumanne November 17.

0 comments: