Beki wa kimataifa wa Brazil anayekipiga katika klabu ya Paris Saint Germain yaUfaransa David Luiz pamoja na mchezaji mwenzake anayeichezea klabu hiyo na timu ya taifa ya Uruguay Edinson Cavani wamegoma kurejea Paris Ufaransa ambapo ni makao makuu ya klabu yao ya PSG na walisafiri kwa muda kwenda kuzitumikia timu zao za taifa.
Wachezaji hao bado hawako tayari kurejea makao makuu ya Ufaransa kutokana na hali ya usalama wa mji huo ambapo jioni ya November 13 lilifanyika shambulio la kigaidi, shambulio hilo lililotokea Ijumaa ya November 13, watu 129 waliripotiwa kupoteza maisha lakini wengi zaidi wamejeruhiwa.
“Paris nina mpenzi wangu ndugu na marafiki, wote hawa wana huzuni na wanaogopa kwa kilichotokea, sijui nini cha kufanya kama nitarejea Paris au la, kuitumikia PSG ni kazi yangu lakini nini kitatokea kama nikirejea Paris” >>> David Luiz
Hata hivyo kikundi cha kigaidi cha ISIS kinatajwa kukiri kuhusika na tukio hilo la kigaidi lililochukua uhai wa watu 129.
0 comments:
Post a Comment