Tuesday, 17 November 2015

Live: Yanayojiri Leo Bungeni Katika Uchaguzi na Kiapo cha Spika wa Binge la 11



Bunge la 11 la Jamhuri ya Muungano linaanza leo Dodoma kwa kusomwa Tangazo la Rais la Kuitisha Bunge, uchaguzi na Kiapo cha Spika, Kiapo kwa wabunge wote
Muda huu tayari wabunge wameanza kuwasili kwenye viwanja vya Bunge na wengi wamo kantini hapa wakipata staftahi kabla ya kuingia rasmi ukumbini.

Update.
Wabunge wengi wanaingia bungeni now harakaharaka maana mida wowote Kikao kitaanza. Changamoto iliyopo ni kuwa.baadhi ya wabunge hasa wapya wamevaa mavazi ambayo sio ya kibunge jambo ambalo ni kinyume na kanuni. Labda ugeni utawaokoa wasitolewe nje

Updates
Katibu wa Bunge Dr Kashililah ndio anaanza kwa kusoma tangazo la Rais kuitisha bunge la 11. Mkutano wa uchaguzi unaanza na Andrew chenge anateuliwa kuwa mwenyekiti wa muda kuongoza uchaguzi wa spika. Chenge kaingia na uchaguzi unaanza kwa wagombea kuitwa kujieleza

Updates
Wagombea wote wameruhusiwa kuingia ndani na wameingia ukumbini isipokuwa Hashim Runngwe ingawa hajajitoa hivyo anaruhusiwa kupigiwa kura bado

Updates
Wagombea wametoka nje na wanaitwa mmojammoja kujieleza kwa dakika tatu na maswali matatu kama yapo
==============
Wanaogombania nafasi ya uspika wanaendelea kuomba kura na sasa ni zamu ya aliyekuwa naibu spika wa bunge la kumi, Job Ndugai. Amesema anaelimu ya kutosha na uzoefu pia yeye ni mbunge mwenzao hivyo anaekaa na mgonjwa ndiye anayejua matatizo ya mgonjwa.

Selasini(Swali): Ni namna gani kama spika utasimamia vyombo mbalimbali vya bunge?

Ndugai: Niwahakikishie taasisi ya bunge naifahamu vizuri ikiwemo vyombo na kamati zake, kwa uzoefu na elimu msiwe na wasiwasi.

Tizeba(Swali): Ndugai! Tukiacha mambo ya utani kati yangu na wewe, ningependa kujua uzoefu unaousema mbona haufanani na umri wako, ningependa kujua umri wako kama hutojali.

Chenge: Hilo sio swali.

Kunchela(Viti maalum Katavi): Kwa tathmini ya bunge lililopita ulionesha ubabe, umejipangaje kuendeleza ubabe huo ukipata nafasi?

Chenge: Hilo sio swali, ni maoni yako.
Wabunge wanaomba utaratibu na Chenge anagoma.

Molell: Baadhi ya wabunge walitoka nje bunge lililopita, Ni kwa namna gani atahakikisha bunge hili

Zitto(Utaratibu): Bunge likishaisha na mambo yake yanaisha, toka maswali yanaanza mwenyekiti umekuwa unaruhusu maswali kwa reference ya mabunge yaliyopita.

Chenge: Silichukui hilo la Zitto Kabwe na Ndugai jibu hilo kwa kifupi

Ndugai: Nawahakikishia bunge la amani, umoja na upendo, nawaomba kura zenu, hapa kazi tu.

Anaefuata sasa ni Ole Medeye kupitia CHADEMA
Medeye: Sheria zinazotungwa na bunge hili ndio msingi wa kugawa haki katika bunge hili, lengo langu la kwanza nitakalolisimamia ni kuhakikisha tunapata katiba mpya. 

 Jambo la pili natambua wa bunge katika kuisimamia serikali, nitaomba kama bunge tufanye marekebisho makubwa.(Muda umeisha) Nawaomba kura zenu ili tuweze kufanya marekebisho hivyo wabunge mnipe fursa, naomba kura.

Bobari(Mchinga): Natambua mgombea ni mzoefu serikalini, unadhani kasi ya bunge hili inahitaji spika wa aina gani kuendana na kasi hii.

Medeye: Wabunge walio wengi ni vijana hivyo mtazamo wa bunge hili ni kesho na sio jana, nikipewa fursa hiyo nina uwezo wa kusimamia bunge hili, dhima yangu mojawapo ni kurekebisha bunge.

Nape: Nakushukuru, naitwa Nape mbunge wa Mtama. Kumbukumbu zinaonyesha ulishawahi kutolewa na ndugu Lema una tuhuma za ubaguzi, sijui tabia hizo umeshaacha!
Chenge: Hilo sio swali

Jaffo: Watanzania wamekubali slogan ya Magufuli ya hapa kazi tu, mbunge amejipanga vipi kuhakikisha tunaenda na kasi.

Medeye: 2010 nilinadi ya ari zaidi lakini hatukuenda na kasi hio, tunachotaka ni serikali kuleta mipango itayoendana na hio Slogan

Wabunge wote saba waliofika kati ya nane wamejinadi kwa wabunge kasoro Hashim Rungwe ambae hajafika lakini katibu wa bunge amesema jina lake litajumuishwa katika wabunge watakaopigiwa kura kwa sababu hajatoa taarifa ya kujiondoa.

Bunge limejiridhisha na idadi ya wabunge waliohudhuria kufikia akidi kwani idadi inayohitajika ili kupiga kura ni nusu ya wabunge wote ambapo wabunge wote wanaotakiwa ni 364 na idadi ya wabunge waliohudhuria ni wabunge 359 hivyo kufikisha akidi.

Karatasi za kupigia kura zinagaiwa kwa wabunge wakiwa kwenye viti vyao na yanatangwazwa marekebisho kwa jina moja lililokosewa ambalo marekebisho yake yalishindwa kufanyika ndani ya wakati.

UPDATE:
-->Mh Job Ndugai ametangazwa rasmi kuwa Spika wa Bunge baada ya kupata kura 254
 

0 comments: