Jina la Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dk. John Pombe Magufulilimeendelea kugusa kwenye vichwa vya habari toka siku ya kwanza aliyoanza kazi yake ndani ya Ikulu Dar es Salaam…
kazi imeendelea mtu wangu, Jumatatu November 9 2015 kaanza na ziara ya kushtukiza Hospitali na kukuta hali isiyo ya kuridhisha kwenye upande wa huduma zinazotolewa.
Taarifa nyingine iliyonifikia kutoka Ikulu Dar es Salaam baada ya ziara hiyo ya Rais JPMinahusu kufutwa kwa Bodi ya Wakurugenzi wa Hospitali ya Muhimbili >>>
‘Leo mchana Rais Dk. MAGUFULI amefanya ziara ya kushtukiza kwenye Hospitali ya Muhimbili, hakufurahishwa na hali aliyoikuta.’ >>> Hii ni kauli kutoka kwa Katibu Mkuu Kiongozi, Balozi Ombeni Sefue.
“Amekuta wagonjwa wamelala chini, mashine hazifanyi kazi na hazijafanya kazi kwa miezi miwili, wakati mashine za Hospitali binafsi zinafanya kazi na wagonjwa wanaelekezwa waende huko, amesikitishwa sana.”- Balozi Ombeni Sefue.
“Rais Dk. MAGUFULI amechukua uamuzi wa kuvunja Bodi ya Hospitali ya Muhimbili na kumwondoa aliyekuwa anakaimu nafasi ya Mkurugenzi Mkuu wa Hospitali, amemhamishia Wizara ya Afya ambapo atapangiwa majukumu mengine huko… Rais amemteua Prof. Lawrence Mseru aliyekuwa akiongoza MOI, kubadili kwenye nafasi ya Kaimu Mkurugenzi Muhimbili.”
Kwenye sentensi nyingine Balozi Ombeni Sefue ametoa maagizo haya toka Ikulu >>>>
“Rais ameagiza ndani ya wiki mbili mashine zote zianze kufanya kazi, vilevile Wizara ya Fedha imetoa Bilioni tatu ili zitengeneze mashine hizo… anachosema Rais MAGUFULI kwamba sasa ni kazi tu sio utani, kila mahali lazima watu wafanye kazi kwa sababu hamjui lini mtakuja kutembelewa bila taarifa… lakini cha muhimu zaidi watu wasifanye kazi kwa kuogopa kwamba Rais atakuja kuwakagua, lakini wafanye kazi kwa sababu ni watumishi wa umma“
0 comments:
Post a Comment