Monday, 16 November 2015

Kuna uwezekano mkubwa kwa Mbwana Samatta kucheza mpira Ulaya …

Mbwana Aly Samatta ni mshabuliaji wa kimataifa wa Tanzania anayekipiga katika klabu ya TP Mazembe ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya KongoSamatta amekuwa akiingia katika headlines kila siku kutokana na uwezo wake akiwa na klabu yake ya TP Mazembena timu ya taifa ya Tanzania Taifa Stars.
Mshambuliaji huyo kwa sasa amekuwa gumzo kila kona ya Afrika, hii inatokana na uwezo wake wa kucheka na nyavu ambao umeisaidia TP Mazembe kutwaa taji la klabu Bingwa barani Afrika sambamba na yeye kutwaa kiatu cha dhahabu kwa kuibuka mfungaji bora wa mashindano hayo.
Samatta kwa sasa amekuwa akihusishwa kwenda kucheza soka katika vilabu kadhaa barani Ulaya licha ya kuwa meneja wake Jamal Kisongo amethibitisha kuwa tayariMoise Katumbi ambaye ni mmiliki wa TP Mazembe ana ofa ya Samatta mezani hivyo kuna kila dalili za jamaa kwenda Ulaya, kuna tetesi za vilabu kadhaa ambavyo huenda Samatta akachezea licha ya kuwa anahusishwa sana kwenda Ufaransa kujiunga na klabu ya Lille.
12oc13-tpma-fcmk_207_1381681076
Hizi ni sababu ambazo zinaashiria safari ya Samatta kwenda kucheza soka Ulaya kuwa imeiva
1- Ametwaa taji la Ligi ya Mabingwa Afrika akiwa na TP Mazembe huku yeye akiwa ni miongoni mwa wachezaji tegemeo kwa timu hiyo, kwani TP Mazembe mara ya mwisho kutwaa taji hilo ilikuwa mwaka 2010.
2- Kuibuka kuwa mfungaji bora wa michuano ya klabu Bingwa Afrika kwa kupachika jumla ya goli nane na kumzidi mshambuliaji wa klabu ya Al Merreikh Bakri Abdel Kader Babekerhivyo kitendo hicho kinamuweka sokono kirahisi.
IMG_20151102_222556
3- Kuwa miongoni mwa wachezaji kumi wanaowania tuzo ya mchezaji bora wa Afrikakwa wachezaji wanaocheza Ligi za ndani ya Afrika kitu ambacho kinamuweka sokoni kwani mawakala pia huwa wanaangalia sana wachezaji wanaofanya vizuri barani Afrikana kuwapeleka kucheza soka Ulaya.
4- Licha ya kutwaa kiatu cha dhahabu kwa kuibuka mfungaji bora wa klabu Bingwa baraniAfrika, bado ana nafasi kubwa zaidi ya kuonesha uwezo wake duniani kwani TP Mazembe itashiriki michuano ya klabu Bingwa Dunia itakayoanza December 10-20 2015Japan hivyo hiyo ni sehemu nyingine itakayomfanya aonekane zaidi.
2732263_full-lnd
5- Kutokea katika gazeti maarufu la Uingereza Dailymail baada ya kuisaidia TP Mazembe kutwaa Ubingwa wa klabu Bingwa barani Afrika kwa kuifunga USM Alger kwa jumla ya goli 4-1, hivyo stori yake kutokea katika gazeti lile ni ishara tosha kuwa kazi yake inatambulika sehemu kubwa zaidi.
Screenshot_2015-11-09-07-21-49 (1)

0 comments: