Picha sio Halisi
Kyela mjini imelipuka kwa shangwe baada ya kusikia mbunge wao hajachaguliwa kuwa waziri mkuu.
Mwakyembe alitumia gia ya kutumwa na Magufuli ili apewe uwaziri mkuu ili kushinda kura ya maoni CCM baada ya kubebwa na viongozi wa chama hapo wilayani kwa ahadi za kumpa Mwenyekiti ukuu wa wilaya akiwa waziri mkuu.
Kwenye uchaguzi mkuu aliendeleza uongo wake kwa kuwaambia wananchi katumwa na Magufuli na Kyela itapata waziri mkuu. Mkuu wa wilaya kwa kushirikiana na mkuu wa polisi wakatumia nguvu kulazimisha ushindi. Kesi ya ushindi wake iko mahakamani Mbeya. Inasemekana mkuu wa wilaya aliahidiwa cheo cha mkuu wa mkoa.
Mwakyembe ameingia kwenye mgogoro mkubwa na vijana wilayani hapa baada ya kutumia visasi kuifungia redio ya Kyela fm ambayo inamilikiwa na mpinzani wake kisiasa na ambayo inasikilizwa sana na wakazi wa Kyela. Pia vijana waliokuwa wanapinga ushindi wake walipigwa vibaya na polisi na wengine mpaka kupewa vilema.
Mwakyembe ambaye wilayani Kyela kapoteza umaarufu kabisa baada ya utendaji wake kuwa mbovu mno. Ana sifa kubwa kitaifa wakati wilayani kwake kashindwa kutatua hata matatizo madogo. Siku hizi kapachikwa jina la Nkurunziza baada ya kuona anang'ang'ania kubaki madarakani.
chanzo kitenge blog
chanzo kitenge blog
0 comments:
Post a Comment