Thursday, 19 November 2015

Lipumba Amtahadharisha Rais Magufuli Kuhusu Dr. Shein Kuhudhuria Bungeni Leo



Aliyekuwa Mwenyekiti wa Chama Cha Wananchi (CUF), Prof. Ibrahim Lipumba, amemtaka Rais John Magufuli kuishauri Tume ya Uchaguzi ya Zanzibar (ZEC) kutangaza matokeo ya uchaguzi wa Zanzibar kabla ya kuhutubia bunge leo jioni, .
 
Akizungumza na waandishi wa habari jana Ofisi Kuu ya chama hicho Buguruni jijini Dar es Salaam Prof. Lipumba alisema, ZEC imebakiza kuhakiki majimbo 14 ambapo haitachukua saa tatu katika kupitia majimbo hayo na kumtangaza mshindi

Profesa Lipumba alisema kuwa uchaguzi huo ulifutwa baada ya kushindwa kwa dhahiri mgombea wa kiti hicho kupitia Chama cha Mapinduzi CCM ndipo hapo vyombo vya dola vikamshinikiza ambapo mwenyekiti watume hiyo alichukua hatua ya kuvunja katiba kwa kufuta uchaguzi huo

Prof. Lipumba amesema kuwa, hulka ya Chama Cha Mapinduuzi (CCM) kuingilia na kuvuruga matokeo sio mara ya kwanza na kwamba walianza mwaka 1995 akitoa mfano Naibu Katibu Mkuu wa chama hicho kuwa aliiandikia barua tume kufuta uchaguzi na agizo hilo kutekelezwa.

Katika  hatua  nyingine, Lipumba  alimtaka  Rais Magufuli kuandaa bajeti upya ambayo ni halisia na inatekelezeka badala ya kutegemea ya mwaka 2015/16 ambayo haiwezi kutekelezeka.

0 comments: