Rais wa jamhuri ya muungano wa Tanzania Dr.John Pombe Magufuli amefuta safari zote za nje za watendaji wakuu wa serikali huku zile zenye ulazima zikitakiwa kutolewa kibali maalum na rais ama katibu mkuu kiongozi ambapo pia ameawataka watendaji hao wakuu wa serikali kufanya ziara za vijijini ili kujionea kero za wananchi na kuweka mikakati ya kuzitatua.
Rais Dr.John Pombe Magufuli akiwa na makamu wake wa rais ametoa maagizo hayo katika mkutano wake alioufanya na watendaji wakuu wa serikali wakiwemo makatibu wakuu na Manaibu wao,Gavana wa Benki kuu pamoja na kamishna mkuu wa mamlaka ya mapato Tanzania TRA.
Katika mkutano huo rais Dr .Magufuli amewataka watendaji hao kuwaachia mabalizi wa Tanzania walioko katika nchi mbalimbali kushughulikia shughuli zote zinazopaswa kufanywa nje ya nchi mpaka hapo atakaposema vinginevyo.
Aidha amemtaka kamishna mkuu wa mamlaka ya mapato Tanzania TRA Rished Bade kusimamia kikamilifu na kwa uadilifu suala la ukusanyaji wa mapato hasa kwa wafanyabiashara wakubwa na wale wanaokwepa kodi bila ya woga wala uonevu ili kuiwezesha serikali kuwa na fedha zitakazowezesha kutatua kero za wananchi kama alivyoahidi katika kampeni zake.
Aidha rais Dr.Magufuli pia ameagiza usimamizi makini na uadilifu katika manunuzi ya serikali ambayo yamekuwa yakitumiwa vibaya na kutoa mwanya kuibia serikali kwa kuongeza bei hata kama bidhaa yenyewe ni ya bei ya chini na kwamba watendaji watakaobainika kufanya ujanja ujanja ama ubadhirifu katika manunuzi watawajibishwa mara moja.
Pia rais Dr.Magufuli ameagiza utekelezwaji wa utoaji wa elimu bure kuanzia darasa la kwanza hadi kidato cha nne kuanzia mapema mwakani na kuagiza suala la mikopo ya wanafunzi wa elimu ya vyuo vikuu lifanyiwe kazi na mipango yake kwa ajili ya utekelezaji ili kuwaondolea kero wanafunzi.
CHANZO IKULU BLOG
0 comments:
Post a Comment