Saturday, 7 November 2015

MGOMBEA URAIS WA FIFA ATAKA TIMU 36 KATIKA KOMBE LA DUNIA

prince ali

Wakati mchakato wa kumpata Rais wa FIFA ukiendelea,mmoja kati ya wagombea wa kiti cha Urais Prince Ali Bin Al-Hussein ametaka idadi ya timu kuongozeka kutoka 32 mpaka 36 katika michuano ya kombe la dunia itakayofanyika mwaka 2026.
Imezoeleka kuwa michuano ya kombe la dunia kuwa na timu 32 na kugawanywa katika makundi 8 lakini Prince Ali anasema kuwaataongeza idadi ya timu endapo atachaguliwa kuwa Rais wa FIFA.
Pince Ali hakuishia hapo anasema kuwa fainali za kombe la dunia za mwaka 2026 zinapaswa kupewa ukanda wa bara la Amerika ya kati na kaskazini CONCACAF.
Tayari nchi za Canada,Marekani na nchi ya Mexico ambayo imeandaa fainali hizo mara mbili zimeonesha nia ya kuandaa fainali za mwaka 2026 na tayari zinajiandaa kupeleka maombi ya kuandaa fainali hizo.
Prince Ali anaielezea kauli yake kwa kusema kuwa”hafanyi siasa katika hili la kuongeza timu katika fainali za kombe la dunia na pia siyo kampeni za uchaguzi bali anafanya hivyo kwa sababu za kimpira”.
Prince Ali pia ameitazama michuano ya vijana na anasema endapo atachaguliwa kuwa Rais wa FIFA basi ataongeza michuano ya dunia ya vijana chini ya miaka 15 katika michuano ya kombe la dunia ya vijana ya FIFA.

0 comments: