Kikosi cha Taifa Stars kinaendelea na kambi yake hapa jijini Johannesburg, Afrika Kusini.
Kwa mujibu wa Kocha Mkuu, Charles Boniface Mkwasa, Stars itafanya mazoezi leo mara moja.
“Mazoezi yatafanyikaa asubuhi tu, taratibu tumeanza kuwapunguzia wachezaji mzigo.
“Tulianza kwa kasi na mazoezi yalikuwa magumu sana kwa kuwa tulitaka wawe vizuri,” alisema Mkwasa.
Stars inajiandaa na mechi dhidi ya Algeria kuwania kucheza Kombe la Dunia hatua ya makundi itakayopigwa Novemva 14 jijini Dar es Salaam.
0 comments:
Post a Comment