Wednesday, 4 November 2015

Watu 60 hawana mahali pa kuishi baada nyumba zao kuezuliwa na mvua Songea.


Watu sitini hawana mahali pakuishi baada ya nyumba kumi na moja kubomoka huku wengine wakijeruhiwa kufuatia mvua kubwa ya mawe iliyonyesha katika kijiji cha Nakahegwa kata ya Mbingamharule Songea vijijini mkoani Ruvuma.
 
ITV imefika eneo la tukio katika kijiji cha Nakahegwa kata ya Mbinga Mharule Songea vijijini mkoani Ruvuma na kushuhudia nyumba zikiwa zimebomoka na migomba ikiwa imeanguka na kuwaacha watu sitini wakiwa hawana mahali pa kuishi kutokana na mvua hizo na hapa wananchi wanaeleza hali ilivyokuwa.
 
Licha ya kuharibu nyumba mvua hizo zimelowanisha mbolea na kuharibu vyakula na kuwaacha wananchi wakiwa hawana vyakula kama wanavyozungumza ambapo wanasema mvua hiyo haijawahi kutokea katika kijiji hicho.
 
Afisa mtendaji wa kijiji cha Nakahegwa Bi. Tumaini simon amethibitisha maafaa yaliyotokana na mvua hiyo ambapo amesema watu wawili waliojeruhiwa kwenye majanga hayo wamelazwa hospitali ya misheni Peramiho.
 

Chanzo  ITV 

0 comments: