Saturday, 7 November 2015

MGAWA WENYEJIKO NA VITU KAMA TUNDU LA CHOO WAZINDULIWA MOSCOW URUSI (Toilet Cafe ?)


Nyumba nyingi huwezi kukutana na jiko lililo karibu kabisa na choo, kwa sababu hata matumizi ya sehemu hizo mbili yako tofauti… vipi hii ya jiko na choo kwenye chumba kimoja je?
Toilet
Kwenye vitu ambavyo vimenishtua leo na hii imo, yani watu wa Moscow Urusi wameona haja ya kuweka mambo tofauti… bango tu linalotangaza biashara limeandikwa Crazy Toilet Cafe, mgahawa ambao usishangae ukaagiza supu na ikaletwa ndani ya bakuli linalofanana na sinki la choo.. kuanzia kiti cha kukalia kina umbile hilo, mpaka mabakuli ya chakula na vyombo vingine viko hivyo !!
ToilET ii
Usishtuke mtu wangu, hapo ni kiti cha mgahawa pamoja na mto wa kuegamia,  alafu mambo mengine ya huduma yanaendelea.
Mgahawa wa aina hii ni wa kwanza kwa nchi za Ulaya, lakini unaambiwa hata Taiwannako uko mgahawa ambao vitu vyake vya ndani vinafanana na sinki la chooni !!
Bango linasomeka hivyo nje ya mgahawa, Crazy Toilet Cafe
Bango linasomeka hivyo nje ya mgahawa, Crazy Toilet Cafe
Kila mtu anakaribishwa kwa huduma poa za msosi, na bei ni ya kawaida kabisa kwa hiyo sio mahali pa kupaogopa… mfano ukafunguliwa mgahawa wa hivi Bongo utatamani kwenda na mtu wako mkaenjoy lunch?
Toi II
Hii hapa video ya Mgahawa wa Crazy Toilet Cafe uliofunguliwa Moscow, Russia..

0 comments: