Saturday, 7 November 2015

Jeshi la Polisi limepiga Marufuku Mikutano ya Kisiasa na Maandamano

Jeshi la Polisi nchini hapa limepiga marufuku mikutano ya hadhara na maandamano ya vyama vya siasa kwa kile ilichoeleza tathimini iliyofanywa na jeshi hilo inaonyesha bado kuna mihemko ya kisiasa ambayo inaweza sababisha uvunjifu wa amani endapo itaruhusiwa kufanyika.

Msemaji wa Jeshi la Polisi nchini ssp Advera Bulimba, amewaeleza waandishi wa habari jijini Dar es salaam kuwa, maombi yote ya kufanya mikutano na maandamano yaliyotolewa na vyama vya siasa vya CCM na Chadema yamezuiliwa mpaka hapo hali itakapotengamaa baadae.

chanzo. Chanel 10


NIONAVYO:Hii inamaanisha nini kuhusu kampeni za uchaguzi mdogo,kuwa kampeni hazitatumia mikutano ya kisiasa?

Hao watu wenye mihemko wapo kiasi gani? Na kwa nini wanamihemko? Kwa sababu wameshinda au kushindwa au kudhulumiwa?

Ningeshauri polisi wetu waendeleze weledi waliouonesha kwenye kulinda mikutano ya kampeni kwa kuwaruhusu watu waandamane au hata kufanya mikutano ili kuwaondolea msongo na kuanza maisha mapya kwa #HapaKaziTu.

0 comments: