Saturday, 7 November 2015

Matokea ya Manchester United Vs West Bromwich na matokeo ya mechi nyingine za Ligi Kuu Uingereza November 7


November 7 Ligi Kuu Uingereza imeendelea tena kwa michezo kadhaa kupigwa katika viwanja tofauti tofauti Uingereza, klabu ya Manchester United iliyokuwa nafasi ya nne katika msimamo wa Ligi Kuu Uingereza ilishuka dimbani kuikaribisha klabu ya West Bromwich Albion katika uwanja wa Old Trafford.
3000 (1)
Kabla ya kucheza mchezo dhidi ya West Bromwich AlbionMan United walikuwa na point 21 na kuwa nyuma ya klabu ya Man City inayoongoza Ligi kwa tofauti ya point 4,Arsenal wakishika nafasi ya pili huku wakiwa sawa kwa point na Man CityLeicester wakiwa nafasi ya tatu kwa point 22 huku Man United wakifunga top 4.
3000
Hata hivyo mchezo huo umemalizika kwa klabu ya Man United kufanikiwa kuibuka na ushindi wa jumla ya goli 2-0 dhidi ya West Bromwich, magoli ambayo yalifungwa na Jesse Lingard dakika ya 52 kipindi cha pili na Juan Mata alifunga goli la pili kwa mkwaju wa penati dakika ya 90 ya mchez0.
Matokeo ya mechi nyingine za Ligi Kuu Uingereza November 7
  • Bournemouth 0 – 1 Newcastle
  • Leicester 2 – 1 Watford
  • Norwich 1 – 0 Swansea
  • Sunderland 0 – 1 Southampton
  • West Ham 1 – 1 Everton

 

0 comments: