Wednesday, 4 November 2015

Mwisho wa uwaziri leo baada ya Mawaziri kuaagizwa Kurejesha Ikulu Magari ya Serikali leo asubuhi kabla ya kuapishwa magufuli

 


Katibu Mkuu Kiongozi, Ombeni Sefue, amewaagiza  Mawaziri na Naibu Mawaziri leo kurudisha magari ya serikali baada ya Rais Mteule, Dk. John Magufuli kuapishwa kwa kuwa ndiyo siku yao ya ukomo wa uongozi.

Jana Balozi Sefue alisema baada ya Bendera ya Rais kuteremshwa na kabla Bendera ya Rais mpya kupandishwa, magari ya mawaziri na Naibu Mawaziri, yatabadilishwa namba kwa kuondoa herufi ya cheo chake (W au NW) na kurejeshwa kwenye namba za serikali (ST).

Balozi Sefue alisema baada ya shughuli hiyo, magari hayo yatawarudisha nyumbani mawaziri na naibu Mawaziri waliomaliza muda wao na kurejeshwa Ikulu tayari kwa ajili ya kupewa mawaziri wapya watakaoteuliwa.

0 comments: