Saturday, 15 February 2014

KLABU AFRIKA: YANGA KUCHEZA COMORO LEO JUMAMOSI, AZAM FC NAO KUCHAPANA JUMAPILI!

>>VISIWANI: KMKM, CHUONI KUPINDUA VIPIGO VIKUBWA??
  
Wachezaji wa Young Africans wakimsikiliza kocha kabla ya kuanza mazoezi leo asubuhi

TIMU 4 za Tanzania Wikiendi hii zipo kwenye Mechi za Marudiano za Raundi ya Awali ya Michuano ya CAF ya CHAMPIONZ LIGI na Kombe la Shirikisho.
WAKATI Yanga inashuka Jumamosi Uwanja wa Sheikh Said Mohamed International, Mitsamihuli, Visiwa vya Comoro kurudiana na Komorozine de Domoni waliyoichapa 7-0, Azam FC wapo Jijini Beira Nchini Msumbiji ambapo Jumapili wanarudiana na Ferroviario da Beira waliyoifunga 1-0 lakini kazi kubwa iko huko Zanzibar ambapo Wawakilishi wa Visiwa hivyo, KMKM na Chuoni, wanatakiwa wapindua vipigo vikubwa walivyovipata kwenye Mechi zao za kwanza walizocheza Ugenini.
Katika Timu hizi za Tanzania, Yanga, ambao wanacheza CAF CHAMPIONZ LIGI, wapo kwenye kazi rahisi kwani wana ushindi mkubwa wa Bao 7-0 walioupata kwenye Mechi ya Kwanza na ni wazi wapo mguu mmoja mbele kukutana na Mabingwa Watetezi wa Afrika, Al Ahly ya Misri, katika Raundi ijayo.
Yanga wapo huko Comoro bila ya Kipa wao Juma Kaseja, ambae ameachwa kwa sababu ni mgonjwa na pia Straika, Jerry Tegete, ambae ilibidi aende Mwanza kumuuguza Mama yake.
Nao Azam FC, licha ya kuifunga Ferroviario da Beira, Bao 1-0 walipocheza Azam Complex huko Chamazi Wiki iliyopita, bado wana kazi kubwa kuhakikisha wanasonga kwenye Michuano hii ya Kombe la Shirikisho ili wakutane na ZESCO ya Zambia kwenye Raundi ijayo.
Huko Zanzibar, Jumamosi, KMKM, ambao wanacheza CAF CHAMPIONZ LIGI, wanapaswa kuifunga Dedebit ya Ethiopia zaidi ya Bao 3 kwani wao walichapwa 3-0 huko Ethiopia Wiki iliyopita.
Na wenzao Chuoni, ambao walipigwa 4-0 na How Mine huko Zimbabwe kwenye Mechi ya Kwanza ya Kombe la Shirikisho, wanapaswa kushinda Bao 5-0 ili wasonge Raundi ya Kwanza.
CAF CHAMPIONZ LIGI
RATIBA
[Kwenye Mabano Matokeo Mechi za Kwanza]
Jumamosi Februari 15
OS Balantas - Guinea-Bissau vs Sewe Sport - Ivory Coast
Steve Biko - Gambia vs Entente Sportive de Sétif – Algeria [0-6, Biko wamejitoa]
Côte d'Or – Seychelles vs Kabuscorp – Angola [1-5]
Komorozine – Comoros vs Young Africans – Tanzania [0-7]
Kampala City Council FC – Uganda vs El Merreikh – Sudan [2-0]
Nkana FC – Zambia vs Mbabane Swallows – Swaziland [0-2]
Flambeau de l’Est – Burundi vs Diables Noirs – Congo [1-0]
Rayon Sports – Rwanda vs AC Leopards de Dolisie – Congo [0-0]
Black Africa – Namibia vs Kaizer Chiefs - South Africa [0-3]
Diamond Stars - Sierra Leone vs Raja Club Athletic – Morocco [0-6]
18:00 ASFA-Yennenga - Burkina Faso vs Diambars – Senegal [0-1]
Kano Pillars FC – Nigeria vs AS Vita Club - Congo, DR [1-3]
Bamako – Mali vs FAR Rabat – Morocco [2-2]
Jumapili Februari 16
Cnaps Sports – Madagascar vs Liga Muculmana de Maputo – Mozambique [0-1]
Mochudi Centre Chiefs – Botswana vs Dynamos – Zimbabwe [0-3]
Lioli – Lesotho vs Primeiro de Agosto – Angola [0-2]
Akonangui - Equatorial Guinea vs Les Astres de Douala - Cameroon [0-0]
Union Sportive Bitam – Gabon vs Gor Mahia – Kenya [0-1]
Foullah Edifice – Chad vs Al Ahli - Benghazi – Libya [0-4]
Douanes Niamey – Niger vs Al Zamalek – Egypt [0-2]
Anges de Notsè – Togo vs Enyimba International FC – Nigeria [1-3]
KMKM Zanzibar - Tanzania vs Dedebit – Ethiopia [0-3]
Barrack Y.C.II – Liberia vs  Asante Kotoko – Ghana [1-2]
Atlabara - South Sudan vs  Berekum Chelsea – Ghana [0-2]
Horoya Athlétique Club – Guinea vs F.C. Nouadhibou – Mauritania [1-1]
Stade Malien de Bamako – Mali vs USM El Harrach – Algeria [2-3]

Related Posts:

0 comments: