Sunday, 13 July 2014

CLUB YA CHELSEA YASAJILI WINGA WA BARCELONA MWENYE KIPAJI CHA HATARI

KLABU ya Chelsea imemsajili kinda wa thamani ya juu kutoka akademi ya Barcelona, winga Josi Quintero.
Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 17 ameposti picha kwenye akaunti yake ya Twitter akisaini Mkataba wa The Blues, akiambatanisha na maelezo kwamba 'furaha kusaini mkataba wangu wa kwanza wa mwanasoka wa kulipwa na klabu kubwa'.
Dole tupu: Quintero akiwa amepozi na jezi za mazoezi za Chelsea 
Talent: Josi Quintero puts pen to paper on his deal with Chelsea
Kipaji: Josi Quintero akisaini Mkataba wa Chelsea

Chelsea inafikiriwa kuzipiga bao klabu za Arsenal na Lyon ambazo nazo pia zilikuwa zinawania saini ya kinda huyo wa Ecuador, ambaye amekua akifanya mazoezi na klabu hiyo tangu Januari. Mchezaji huyo alikuwa benchi wakati timu ya vijana ya Chelsea chini ya umri wa miaka 21 inacheza mechi ya kirafiki dhidi ya Sutton United Jumamosi.

Related Posts:

0 comments: