Wednesday, 12 February 2014

COPPA ITALIA: FIORENTINA YATINGA FAINALI!!

>>KUCHEZA NA NAPOLI AU AS ROMA!
COPPA_ITALIA_2014BAO mbili za Manuel Pasqual na Juan Cuadrado zimeipeleka Fiorentina Fainali ya Coppa Italia baada ya kuifunga Udinese Bao 2-0 hapo jana na kusonga kwa Jumla ya Bao 3-2.
Katika Mechi ya Kwanza ya Nusu Fainali, Udinese ilishinda Bao 2-1.
Kwenye Fainali, itakayochezwa Mei 3, Fiorentina itamvaa Mshindi kati ya AS Roma au Napoli ambao wanarudiana Leo huku Roma wakiwa mbele kwa Bao 3-2 walizoshinda kwenye Mechi ya Kwanza.
Bao la Kwanza la Fiorentina lilifungwa katika Dakika ya 14 kwa shuti kali la Manuel Pasqual lililopiga Posti ya juu na kutinga na la Pili lifungwa katika Dakika ya 61 na Cuadrado pia kwa kigongo kikali.
VIKOSI:
Fiorentina: Neto; Diakite, Rodriguez, Savic (Compper 60); Pasqual, Pizarro, Aquilani, Mati Fernandez, Cuadrado; Joaquin (Vargas 89), Matri (Matos 56)
Udinese: Scuffet; Heurtaux, Danilo, Domizzi; Widmer, Pinzi (Muriel 56), Allan, Gabriel Silva (Yebda 91); Fernandes, Pereyra; Di Natale (Nico Lopez 80)
Refa: Massa
COPPA ITALIA
RATIBA:
[Saa za Bongo]
Jumatano Februari 12
22:45 SSC Napoli v AS Roma [Mechi ya Kwanza 2-3]
FAINALI
Mei 3
Fiorentina v Napoli/ AS Roma [Stadio Olimpico]

Related Posts:

0 comments: