Wednesday, 12 February 2014

KLABU AFRIKA: AZAM IMEONDOKA LEO KUELEKEA MSUMBJI NA YANGA KUONDOKA KESHO!

Timu ya Azam imeondoka leo alfajiri (Februari 12 mwaka huu) kwenda Beira, Msumbiji kwa ajili ya mechi ya marudiano ya Kombe la Shirikisho dhidi Ferroviario da Beira itakayochezwa Jumamosi. Msafara wa timu hiyo unaongozwa na mjumbe wa Kamati ya Utendaji ya TFF, James Mhagama.
Naye mjumbe wa Kamati ya Utendaji ya TFF, Nassib Ramadhan ataongoza msafara wa timu ya Yanga inayoondoka kesho mchana kwenda Comoro kwa ajili ya mechi ya marudiano ya Ligi ya Mabingwa Afrika dhidi ya Komorozine itakayochezwa Jumamosi.

Related Posts:

0 comments: