Dhoruba kali ya majira ya baridi kali
imesababisha zaidi ya watu 300,000 eneo la kusini mashariki mwa Marekani
kukosa umeme wakati dhoruba hiyo ikielekea eneo la kati ya Atlantic na
sehemu za kaskazini mashariki mwa taifa hili.
Dhoruba imesababisha kunyesha kwa
darzeni ya sentimeta za theluji kote katika eneo la Washington DC hapo
Alhamis. Wakati katika baadhi ya maeneo ya Washington imeripotiwa kuwepo
mpaka sentimeta 46 za theluji.
Serikali kuu imefungwa pamoja na
darzeni ya serikali za mji na mashule. Huko North na South Carolina,
dhoruba imesababisha barabara ndogo na barabara kuu hazipitiki na
kulazimisha madereva kuacha magari yao.
Watabiri wa hali ya hewa wamesema Carolina zote mbili zilitarajiwa kupata zaidi ya sentimeta 20 za barafu na theluji hadi Alhamis asubuhi baada ya kupata mchanganyiko wa theluji na mvua hapo Jumatano.
Hali ya hewa imesababisha maelfu ya safari za ndege kufutwa kwa muda, abiria kukwama kwenye viwanja vya ndege. Darzeni ya vifo vimeripotiwa kusababishwa na dhoruba ikiwemo watu watatu kufariki wakati gari la kubeba wagonjwa lilipoteleza kwenye barabara zilizokuwa na barafu huko Texas.
Chanzo, voaswahili.com
0 comments:
Post a Comment