Wachezaji wa Young Africans wakiwa mazoezini
Young
Africans Sports Club wawakilishi wa Tanzania bara kwenye mashindano ya
Klabu Bingwa Afrika kesho watakwea pipa saa 6 kamili mchana kuelekea
Visiwa vya Comoro tayari kwa ajili ya mchezo wa marudiano dhidi ya timu
ya Komorozine de Domoni utakaofanyika siku ya jumamosi katika Uwanja
wa stade International Said Mohamed Cheik Mitsamiouli.
Kikosi cha mholanzi Hans Van der Pluijm kimekua kikifanya mazoezi
asubuhi na jioni katika Uwanja wa Karume makao makuu ya TFF kwa ajili ya
kujiandaa na mchezo huo wa marudiano ambao ni muhimu kwa Young Africans
kuendelea kufanya vizuri na kuweza kusonga hatua inayofuata.
Young
Africans inatarajiwa kuondoka na shirika la ndege la Precision majira
ya saa 6 kamili mchana na kuwasili Visiwa vya Comoro majira ya saa 8
mchana ambapo kikosi kitaelekea hotelini kupumzika kabla ya jioni
kufanya mazoezi mepesi.
Katika
mchezo wa awali uliochezwa mwishoni mwa wiki Young Africans iliibuka na
ushindi wa mabao 7-0 dhidi ya Komorozine mabao yaliyowekwa wavuni na
Mrisho Ngasa (3), Didier Kavumbagu (2), Nadir Haroub (1) na Hamis Kiiza
(1).
Msafara unatarajia kuwa na watu 30 wakiwemo wachezaji 19 Benchi la Ufundi saba (7) pamoja na viongozi wanne (4)
Magoikipa ni: Deogratias Munish "Dida" na Ally Mustafa "Barthez"
Walinzi: Juma Abdul, Mbuyu Twite, Oscar Joshua, David Luhende, Nadir Haroub "Cannavaro", Kelvin Yondani na Rajab Zahir
Viungo: Athuman Idd "Chuji", Frank Domayo "Chumvi", Haruna Niyonzima, Hassan Dilunga na Hamis Thabit
Washambuliaji: Hamis Kiiza, Didier Kavumbagu, Said Bahanuzi, Saimon Msuva na Mrisho Ngasa
Benchi la Ufundi:
Kocha Mkuu - Hans Van der Pluijm
Kocha Msaidizi - Charles Mkwasa
Kocha wa Makipa - Juma Pondamali
Daktari wa Timu - Dr Suphian Juma
Meneja - Hafidh Saleh
Mtunza Vifaa - Mahmoud Omar "Mpogolo"
Mchua Misuli - Jacob Onyango
Viongozi
Aaron Nyanda - Kamati ya Utendaji
Baraka Kizuguto - Afisa Habari
Mohamed Bhinda - Kamati ya Utendaji
Ramadhan Nassib - Mkuu wa Msafara kutoka TFF
0 comments:
Post a Comment