Kwenye
gazeti la Mwananchi la leo nimesoma habari muhimu sana kitaifa. Hakika,
kwanza sikuamini macho yangu. Nikasoma mara ya pili.
Waziri Anna Tibaijuka akiongea na wananchi wa Kapunga kule Mbarali, Mbeya, ameripotiwa akitamka kuwa "Serikali itaendelea kuzungumza na mwekezaji na wananchi ili kumaliza mgogoro, mwekezaji ni mzuri lakini wapo wananchi wakorofi".
Na niweke wazi kuwa Mbarali ndiko iliko asili yangu na hivyo si kwamba kauli ya waziri imenigusa kwa sababu hiyo bali naliona tatizo kubwa kitaifa kama tuna waziri anayediriki kusema aliyoyasema, tena hadharani.
Ndio,
Kama haya kayasema Waziri ukweli afanye uungwana kuwaomba radhi wananchi.
Maana, anaotaka kuzungumza nao tayari ameshawahukumu. Na kama Waziri anamwona mwekezaji ni mzuri aendelee kunywa nae chai maana Waziri ameshachagua upande kwenye mgogoro anaotaka kuhusuluhisha.
Waziri Tibaijuka anajua kuwa suala la ardhi ni nyeti na linahusu uhai wa watu. Na kama waziri anataka kupiga hatua kwenye kuipata suluhu aanze kwa kufuta kauli yake; kuwa mwekezaji ni mzuri na kuna wananchi wakorofi. Na huko pia ni kuwaomba radhi wananchi wa Mbarali.
Maggid Mjengwa,Dar es Salaam.

0 comments:
Post a Comment