Rwanda imeelezea mshangao wake kuona uvumi huo ukizagaa, huku
raia wa mashariki ya Congo wakiandamana wakionyesha furaha kuhusiana na
na taarifa isiyokua ya kweli.
Afisa m'moja anaefanya kazi kwenye Ikulu ya rais wa Rwanda, amefahamisha
AFP kwamba taarifa ya kifo cha rais Paul Kagame ilikua uvumi mtupu.
“ Rais wakati huu tunaongea, anakutana kwa mazungumzo na wanafunzi wa
chuo kikuu kutoka Marekani. Muko huru kuja kuhudhuria kikao hicho, na
muweze kukutana nae, ameendelea kusema afisa huyo.
Paul Kagame, mwenye umri wa miaka 56, ni rais wa Rwanda tangu mwaka wa
1994, baada tu ya waasi wa RPF kushinda jeshi la Rwanda lilokua
likimuunga mkono rais Juvenal Habyarimana. Chanzo cha kushindwa kwa
jeshi la Rwanda ni mauaji ya kimbari, ambayo lilihusishwa jeshi hilo.
Watu laki nane, wengi wao kutoka jamii ya watutsi waliuawa.
Wafuasi wa rais Paul Kagame wanamsifu kwamba ni mtu mwenye mtazamo
katika masula ya uchumi, na lengo lake ni kuliendeleza taifa la Rwanda,
huku wapinzani wake wakimtuhumu kujihusisha na tabia mbovu ya kufuta
vyama vya upinzani.
Paul Kagame amevaa lawama, kwa mujibu wa Jumuiya ya Kimataifa,
kutokana na kuunga mkono makundi ya wapiganaji mashariki mwa Jamhuri ya
Kidemokrasia ya Congo, licha ya kua Kigali imeendelea kukanusha madai
hayo.
0 comments:
Post a Comment