Monday, 13 January 2014

TAARIFA RASIM MSHINDI BALLON D'OR - CRISTIANO RONALDO….NI MCHEZAJI BORA IDUNIAN 2013

>>RONALDO AWABWAGA MESSI & RIBERY!!
>>LEJENDARI PELE APEWA ‘TUZO MAALUM’, HAKUWAHI KUTWAA Ballon d’Or KWA SABABU TU……HAKUWEPO ULAYA!!!!!
>>SERGIO RAMOS: KADI ZA NJANO 142, NYEKUNDU 18…YUPO KIKOSI CHA DUNIA!!!
RONALDO_NA_TUZOUsiku wa leo, huko Kongresshaus, Zurich, Nchini Switzerland, FIFA ilikuwa na Tafrija maalum ya kutunukia Watu mbalimbali Tuzo na Mchezaji Bora Duniani, alietwaa Tuzo ya FIFA Ballon d'Or ni…. CRISTIANO RONALDO….NI BORA DUNIANI!!!
Hii ni mara ya Pili kwa Cristiano Ronaldo, ambae sasa anaichezea Real Madrid na ni Nahodha wa Nchi yake Portugal, kutwaa Tuzo hii na mara ya kwanza ilikuwa ni Mwaka 2008 wakati akiwa na Manchester United.
Kwa kutwaa Tuzo, Ronaldo amewabwaga Lionel Messi, Mshindi kwa Miaka minne iliyopita, na Franck Ribery wa France na Klabu ya Bayern Munich.
RONALDO-PORTUGAL-SHANGILIANae Lejendari wa Soka Duniani kutoka Brazil, Edson Arantes do Nascimento ' Pele', ambae hakuwahi kutwaa Ballon d'Or kwa vile tu enzi zake ilikuwa ikipewa kwa Wachezaji wa Ulaya tu, leo amepewa Tuzo Maalum ya FIFA.
Akiipokea, Pele, huku akitokwa Machozi, alinena: “Niliahidi Familia yangu sitatokwa na Machozi lakini nimeshindwa kujizuia. Kwanza namshukuru Mungu kwa kunipa afya ya kucheza Miaka mingi. Nilikuwa na wivu na wale waliokuwa wakitwaa Ballon d'Or kwa sababu sikushinda, kwa sababu sikucheza Ulaya”. Sasa nina Kombe langu!”
WASHINDI WA TUZO MBALIMALI:
FIFA/FIFPro Kombaini ya Dunia [Kikosi Bora cha Wachezaji 11]
-FIFPRO WORLD XI
KIPA:
Manuel Neuer (Bayern Munich and Germany)
MABEKI:
Dani Alves (Barcelona and Brazil)
Philipp Lahm (Bayern Munich and Germany)
Thiago Silva (Paris St-Germain and Brazil)
Sergio Ramos (Real Madrid and Spain)
VIUNGO:
Xavi (Barcelona and Spain)
Andres Iniesta (Barcelona and Spain)
Franck Ribery (Bayern Munich and France)
MASTRAIKA:
Cristiano Ronaldo (Real Madrid and Portugal)
Zlatan Ibrahimovic (Paris St-Germain and Sweden)
Lionel Messi (Barcelona and Argentina)
**KIBWAGIZO:
-Kabla ya leo, haijawahi kutokea Mchezaji kutoka Bundesliga au Ligue 1 ya France akawemo kwenye FIFA/FIFPro Kombaini ya Dunia
-Kwa Mwaka wa Pili mfululizo, hamna Mchezaji wa Ligi Kuu England kwenye Timu hii ya Dunia na Wachezaji wa Manchester United, Nemanja Vidic na Wayne Rooney, ndio walioteuliwa kwa mara ya mwisho Mwaka 2011.
-Sergio Ramos: Kadi za Njano 142 na Kadi Nyekundu 18 lakini YUPO KIKOSI CHA DUNIA!
FIFA Tuzo ya Rais
-Jacques Rogge, Rais wa zamani wa Kamati ya Kimataifa ya Olimpiki
FIFA Kocha Bora Timu za Wanawake
-Silvia Neid [Germany]
FIFA Kocha Bora Timu za Wanaume
-Jupp Heynckes [Bayern Munich-kabla hajastaafu Mwezi Mei]
FIFA Tuzo ya Uchezaji wa Haki
- AFGHANISTAN: Nchi iliyokumbwa na Vita kwa muda mrefu
FIFA Tuzo ya Puskas [Goli Bora]
- Zlatan Ibrahimovic [Kwa Goli la Tikitaka aliloifunga England]
FIFA Tuzo Maalum
- Edson Arantes do Nascimento ' Pele'
FIFA Mchezaji Bora Kinamama
- Nadine Angerer (Kipa wa Germany)
FIFA Ballon d'Or
- CRISTIANO RONALDO

Related Posts:

0 comments: