Uganda ilikua kwenye uchaguzi mkuu wa kumchagua Rais na Wabunge juzi ambapo matokeo ya awali yalianza kutolewa kuanzia jana lakini leo matokeo kamili yametolewa naYoweri Museveniambaye amekuwepo kwenye kiti cha Urais tokamwaka 1986ametangazwa mshindi huku mpinzani wake mkuu ambaye ni Kizza Besigyeakikataa matokeo hayo aliyoyaita ya wizi wa kura.
Kituo cha TV cha NBS kimeripoti kwamba huduma za Taxi mitaani, mitandao ya kijamii na huduma za benki za simu za mkononi zimerejea baada ya serikali kuamuru juzi kila kitu kizimwe kuanzia Facebook, Twitter, Whatsapp.Rais Museveni baadae alihojiwa na kusema mitandao ya kijamii ilizimwa kwa muda mfupi tu na watu hawakutakiwa kuwa na hofu sababu ilifanywa ili kuzuia upotoshaji wa taarifa tu ambao umekua ukifanywa mara kwa mara.
Rais Museveni alipokutana na Viongozi waangalizi wa uchaguzi Mzee Obasanjo na Banda nyumbani kwa Rais eneo la Rwakitura.
0 comments:
Post a Comment