Wednesday, 17 February 2016

Kamishna wa Elimu Awavua Madaraka Wakuu Watatu wa Vituo vya Elimu ya Watu Wazima Dar, Dodoma na Mwanza

 


Kamishna  wa Elimu, Teknolojia, Sayansi na Ufundi, Profesa Eustella Balamsesa amemuagiza Mkurugenzi wa Elimu ya Watu Wazima, Fedelis Mafumiko kuwavua madaraka Wakuu Watatu (3) wa vituo vya  Elimu ya Watu Wazima kutokana na kukiuka utaratibu wa kuchagua wanafunzi wanaojiunga kidato cha kwanza kuwaingiza katika Mfumo wa Elimu ya Watu Wazima.

Profesa Eustella ameyasema hayo leo wakati alipokutana na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam .

Amesema kuwa wakufunzi hao wamekuwa wakishirikiana na Halmashauri baada ya kuchagua wanafunzi wa kidato cha kwanza ambao wamefanya vizuri wao huchukua wanafunzi waliofeli na kuwapeleka katika shule za serikali wakidai kuwa wanafunzi wamechaguliwa katika chaguo la pili.

Baada ya kuchaguliwa wanafunzi hao wakifika shule wanadaiwa ada wakati serikali imesema elimu  ni  bure, hali inayowachanganya  wazazi.

Wakuu wa vituo waliovuliwa madaraka ni Wotugu Mganda (Dar es Salaam), Senorina Kateule (Dodoma),Steward Ndandu Geita na (Mwanza).

Profesa Eustella amesema kuwa wakufunzi hao wamekuwa wakidandia matokeo ya kidato cha kwanza kwa kufanya upotoshaji kwa wazazi wakati wanafunzi wanaosoma katika elimu ya watu wazima ni hiari kutokana  na sera ya elimu.

Wanafunzi ambao wamechaguliwa kwa mwaka huu wamekuwa wakidai ada ya sh. 80,000 hadi 250,000 na ndipo malalamiko yakaanza kwa wazazi baada ya kudaiwa ada hiyo.

Profesa Eustella, amesema kuwa mmoja wanafunzi katika Mkoa wa Dar es Salaam aliambiwa amefaulu katika chaguo la pili katika shule ya sekondari ya Oasterbay .Baada ya kufika shuleni, mwanafunzi huyo alikuta mambo tofauti kwa kudaiwa ada na kuambiwa awasiliane na Taasisi ya Elimu ya Watu Wazima.

0 comments: