BARAZA LA MITIHANI LA TANZANIA
MATOKEO YA KIDATO CHA NNE (CSEE) 2015
Baraza la Mitihani la Tanzania limekuwa likipigiwa simu na watu mbalimbali
wakiomba ufafanuzi kuhusu taarifa zinazosambazwa kwenye mitandao ya
kijamii kuwa Wizara ya Elimu, Sayansi, Teknolojia na Ufundi imetangaza
kuwa matokeo ya Mtihani wa Kidato cha Nne (CSEE) 2015 yamezuiwa
kwa muda hadi tarehe 08/03/2016.
Baraza la Mitihani la Tanzania linapenda kuwajulisha watahiniwa na umma
kwa ujumla kuwa taarifa hizo ni za UONGO na zinalenga kupotosha umma
na kuleta taharuki.
Hivyo, Baraza linaomba umma kuzipuuza taarifa hizo kwa kuwa Wizara
haijasitisha utoaji wa matokeo hayo. o. Matokeo yatatangazwa mara tu
mchakato utakapokamilika.
Imetolewa na,
AFISA HABARI NA UHUSIANO
Tuesday, 16 February 2016
HOME »
» NACTA YAKANUSHA KUTANGAZWA KWA MATOKEO YA KIDATO CHA NNE2015
0 comments:
Post a Comment