Ndugu zangu,
Nimepata kusema, kuwa haiyumkini
Majaji wetu hawa wazaliwa na wazalendo wa nchi hii wakawa wote wana
matatizo katika kufikiri kwao; Jaji Francis Nyalali, Jaji Robert
Kissanga, Jaji Joseph Warioba na Jaji Augustine Ramadhan . Na nikamsahau
Jaji Mark Bomani. Kwamba wote hawa, na katika nyakati tofauti,
wamependekeza mfumo wa Serikali Tatu ili kuunusuru na kuuimarisha
Muungano wetu.
Nahofia, kuwa baadhi ya wanasiasa wetu
ndio wenye matatizo katika kufikiri kwao. Kwamba wanaangalia kwanza ni
mfumo gani wa Serikali utakaowanufaisha wao binafsi, makundi yao na
vyama vyao kwa kuangalia namna watavyoshinda chaguzi za kisiasa na
kushika madaraka.
Wanaangalia zaidi leo na kesho. Kwao kesho kutwa na mtondogoo ni mbali sana.
Naam, tumwamini nani? Maana, iliimbwa, kuwa ' Mwanasiasa' ni ' kigeugeu! Na Jaji naye....?Maggid Mjengwa,
Bagamoyo.0754 678 252.
0 comments:
Post a Comment