Taarifa zilizochapishwa kwenye ZanziNews.com
jioni hii zinasema kuwa juhudi za wananchi na vyombo husika mpaka sasa
zimefanikiwa kuwapata wananchi wanne wakiwa hai na miili ya watu watano
walioaga dunia (wanawake wawili na wanaume watatu). Miili ya maiti
imehifadhiwa katika hospitali ya Mnazi Mmoja. Serikali itaandaa
utaratibu wa kawaida kwa maiti kuzikwa ama kupewa jamaa zao. Kapteni Nassor Abubakar Khamis ameshikiliwa na jeshi la Polisi kwa mahojiano.
Zoezi la uokozi limesitishwa katika eneo la ajali kutokana na giza hadi hapo kesho asubuhi.
Kutokana na kuwepo kwa taarifa za
kukanganya ambapo baadhi ya abiria wanadai kutokuwaona ndugu zao 7 kwa
kuwa walianguka kwenye maji baada ya MV Kilimanjaro kukumbwa na dhoruba
na hadi sasa hawajaonekana; Huku nahodha wa boti hiyo akikaririwa kusema
kuwa hakuna yeyote aliyeanguka ama kuachwa
katika eneo la mkondo wa maji wa Nungwi; Wakati kamishna wa
polisi Zanzibar Hamdan Makame amesema zipo ripoti ambazo
hazijathibitishwa kuhusu watu 4 waliolazwa katika kituo cha afya cha
Nungwi baada ya kuokolewa;Blog ya Zanzibar Islamic News inaripoti kuwa Waziri wa Miundombinu na Mawasiliano Rashid Seif Suleiman amsesema tayari kundi la wazamiaji tayari limekwenda katika eneo la ajali. Waziri Seif amesema kamati ya ulinzi na usalama imekutana mchana huu na kujadili tukio hilo kabla ya kuelekea eneo la tukio kushirikiana na wataalam wengine kuwatafuta watu hao.
Nalo Jeshi la polisi Zanzibar kwa kushirikiana na Jeshi la polisi Makao makuu Dar es salaam wametuma helkopta katika eneo la tukio ili kubaini watu ambao wanadaiwa kuzama katika eneo hilo.
Mkurugenzi wa Usafiri wa Baharini (ZMA) Mhandisi Abdi Maalim amesema mabaharia walianza kazi ya kuwatafuta watu wanaosadikiwa kuzama majira ya alasiri leo kwa kushirikiana na mabaharia wa kujitolea.
Naibu Mkurugenzi wa Upelelezi Makosa ya Jinai Zanzibar DCI Yussuf Ilembo amesema uhakiki wa majina ya wahanga bado unaendelea ili kupata majina yao na umri wao kwa vile kuna meli mbili zilisafiri kwa wakati mmoja.
Taarifa
zilizotolewa mchana wa leo kupitia vyombo mbalimbali vya habari zilisema
kuwa mnamo wa majira ya saa tano adhuhuri ya leo, boti ya MV
Kilimanjaro II mali ya kampuni ya Azam Marine, ilipatwa na dhoruba
katika eneo la Nungwi wakati ikitokea Pemba kuelekea Unguja na kwamba
abiria wapatao kumi hivi walianguka majini na kutupiwa maboya ya
kujiokoa.Msemaji wa Polisi Zanzibar amekiri kutokea kwa
dhoruba hiyo iliyosababishwa na upepo mkali ulioipiga boti hiyo
iliyokuwa na abiria 369, watoto 60 na mabaharia 8 na kisha baadhi ya
abiria kutupa maboya matano baharini bila ya maelekezo kutoka kwa
nahodha wala mabaharia wa boti hiyo.
Lakini msemaji huyo amekaririwa akitamka kuwa kwa mujibu wa
nahodha Aboubakar wa chombo hicho, hakuna mtu yeyote aliyedondoka ama
kuachwa katika eneo la dhoruba na boti ilifanikiwa kutua nanga salama u
salmin katika bandari ya Zanzibar mwendo wa saa sita kasoro mchana.
0 comments:
Post a Comment