>>MOURINHO ADAI ROONEY ATAIHAMA MAN UNITED!!
>>ROBIN VAN PERSIE: DAVID MOYES ASEMA STRAIKA BURDANI UNITED!
>> ROBERTO DE FANTI: AONDOLEWA SUNDERLAND!
SOMA ZAIDI:
MOURINHO ACHEKA MADAI ALILIA ALIPOTOSWA NA MAN UNITED!!
Katika Kitabu kilichoandikwa na Diego Torres kiitwacho 'Prepare to Lose: The Mourinho Era' [‘Jitayarishe
Kushindwa: Zama za Mourinho’] inadaiwa kuwa Mourinho alilia na
kububujikwa Machozi mengi baada kuambiwa Mrithi wa Ferguson ni Moyes na
kuuchukulia uteuzi huo kama usaliti toka kwa ‘Rafiki yake’ Sir Alex
Ferguson.
Akizungumzia madai hayo, Mourinho
amesema: “Nadhani Mtu alieandika Kitabu hico asiandike Vitabu. Aandike
Vitabu vya Watoto akitumia ubunifu wake!”
Wakati huo huo, Mourinho amedai Wayne Rooney atahama Man United lakini hataenda Chelsea.
Mapema mwanzoni mwa Msimu, Chelsea
ilitoa Ofa kadhaa kutaka kumnunua Rooney na zote kukataliwa na Man
United ambao walisisitiza Staa huyo hauzwi kwa Bei yeyote ile.
Akipiga dongo hilo huku Chelsea na Man
United zikielekea kwenye Mtanange kati yao wa Ligi Jumapili Uwanjani
Stamford Bridge, Mourinho amesema Rooney ataondoka Old Trafford lakini
hatauzwa kwa Klabu yeyote ya Ligi Kuu England kwa vile Man United ina
Msimamo wa kutouzia Wapinzani wake Mastaa wake.
ROBERTO DE FANTI: AONDOLEWA SUNDERLAND!
Sunderland imetengana na Mkurugenzi wao wa Soka Roberto De Fanti ambae aliteuliwa wadhifa
huo Juni 2013.
De Fanti alijiunga na Sunderland mapema Mwaka Jana mara baada ya Paolo Di Canio kuteuliwa kama Meneja.
De Fanti alibakia Stadium of Light baada Di Canio kutimuliwa Mwezi September baada kusimamia Gemu 13 tu.
Chini ya usimamizi wa De Fanti, Sunderland ilisaini Wachezaji 14 mwanzo wa Msimu huu na kutumia karibu Pauni Milioni 19.
Miongoni mwa Wachezaji hao wapya ni
Straika kutoka AZ Alkmaar, Jozy Altidore, Mchezaji wa Kimataifa wa
Italy, Emanuele Giaccherini na Kipa kutoka Arsenal, Vito Mannone.
Baada Di Canio kufukuzwa, Wasaidizi wake
wote, Fabrizio Piccareta, Kocha wa Timu ya Kwanza, Domenico Doardo,
Kocha wa Makipa, na Makocha wa Viungo, Claudio Donatelli na Giulio
Viscardi, wote waliondoka isipokuwa De Fanti alibaki.
Hivi sasa Sunderland ipo chini ya Meneja
Gus Poyet na wapo Nafasi ya 19 kwenye Msimamo wa Ligi lakini wapo
kwenye Nusu Fainali ya Capital One Cup wakiwa wanaongoza Bao 2-1 baada
ya kuifunga Man United katika Mechi ya Kwanza na Jumanne Januari 22
wanarudiana Old Trafford.
ROBIN VAN PERSIE: DAVID MOYES ASEMA STRAIKA BURDANI UNITED!
Zipo ripoti za chinichini kuwa Van
Persie, aliesainiwa kwa Pauni Milioni 24 kutoka Arsenal na Sir Alex
Ferguson, amekuwa hana raha tangu Ferguson astaafu.
Lakini Moyes amesema: "Madai hayo ni mbali sana na ukweli!"
Katika Kitabu cha Maisha yake, Sir Alex
Ferguson aliandika kuwa alimwomba radhi Robin van Persie kwa kustaafu
mapema kwani alipomsaini alimhakikishia kuwa hatastaafu karibuni.
Moyes amefafanua: “Nimesema sana kwamba
haya madai hayana ukweli lakini Watu hawataki kuandika au kusikia.
Lakini huo ndio ukweli. Watu wengi wanajua mie ni mkweli na naongea moja
kwa moja. Ingekuwa lipo tatizo mie ningekuwa wa kwanza kusema. Tuna
uhusiano mzuri na Robin kama vile Wachezaji wengine. Lakini kama mambo
hayaendi vizuri, Watu, kwa sababu zao, wanafikiri mie na Robin hatuna
uhusiano mzuri.”
Kwenye Msimu wake wa kwanza na Man
United kama Meneja, David Moyes ameiongoza Klabu hiyo kutinga Raundi ya
Mtoano ya Timu 16 ya UCL, UEFA CHAMPIONZ LIGI pamoja na Nusu Fainali ya
Kombe la Ligi, Capital One Cup, lakini kwenye Ligi Kuu England, ambapo
wao ndio Mabingwa Watetezi, wapo Pointi 11 nyuma ya Vinara Arsenal.
Jumapili, Man United wanasafiri kwenda
Stamford Bridge kucheza na Chelsea na kabla Mechi hiyo kuanza, wanaweza
kujikuta wako Pointi 14 nyuma ya Arsenal ambao wanacheza Jumamosi na
Fulham Uwanja wa Emirates.
Kwenye Mechi na Chelsea, Man United itawakosa Mastraika wao wakubwa, Van Persie na Wayne Rooney, ambao ni Majeruhi.
Van Persie hajaichezea Man United tangu Desemba 10 walipocheza Mechi ya UCL na kuifunga Shakhtar Donetsk Bao 1-0.
0 comments:
Post a Comment