Mkuu wa Mkoa wa Iringa, Amina Masenze
Katibu wa Chama cha Wamiliki wa Nyumba za Kulala Wageni na Hoteli mkoani Iringa (Iloha) Adam Lameck amesema wafanyabiashara wa huduma hizo wamekataa kulipa tena ushuru wa hoteli hadi watakapoonana na uongozi wa mkoa.
Akizungumza leo katika mkutano wao alisema watalazimika kusitisha utoaji huduma kutokana na mlolongo wa kodi.
“Endapo hatutasikilizwa, tunafunga biashara zetu mpaka hapo tutakapopata muafaka,” alisema.
Mmiliki wa Nyumba ya Wageni, Zakaria Mdeka alisema tangu mwaka 2008 kodi hiyo ilifutwa lakini wao waliendelea kulipa kwa asilimia 10 bila kuzingatia mmiliki anaingiza shilingi ngapi.
Wafanyabiashara hao wamedai wamekuwa wakitozwa mlolongo mkubwa wa kodi zaidi ya 23 ambazo zote zinatakiwa kulipwa bila kuzingatia mmiliki anapata faida kiasi gani.
0 comments:
Post a Comment