Kamanda
wa polisi mkoa wa Singida, SACP Geofrey Kamwela,akitoa taarifa kwa
waandishi wa habari (hawapo kwenye picha) juu ya kifo cha Mwanaume
aliyeuwawa na mkewe kwa kupigwa na kipande cha mti kichwani.(Picha na
Nathaniel Limu).
.kosa alichukua shilingi 25,000 tu bila idhini
Na Nathaniel Limu, Singida
MKULIMA
na Mkazi wa kijiji cha Ntewa, Kata ya Ntuntu tarafa ya Munghaa wilaya
ya Ikungi mkoani Singida,Juma Abdallah (25) amefariki dunia baada ya
kupigwa na mke wake Veronika Hamisi (25) kichwani katika paji la uso na
na kufariki papo hapo.
Kamanda
wa Jeshi la Polisi Mkoa wa Singida,SACP Geofrey Kamwela amesema tukio
hilo limetokea januari mbili mwaka huu saa saba mchana huko katika
kijiji cha Ntewa.
Amesema
siku ya tukio katika muda huo wa saa saba mchana wanandoa hao walirejea
nyumbani kwao wakitokea kwenye klabu cha pombe za kienyeji aina ya
mtukuru.
“Wanandoa
hao vijana wakiwa nyumbani kwao,Juma alichukua pochi ya mke wake
Veronica na kuchukua bila idhini shilingi 25,000 zilizokuwa
zimehifadhiwa kwenye pochi hiyo”,amesema.
Kamanda
Kamwela amesema baada ya Juma kuchukua fedha hizo bila idhini mke wake
alimsihi sana azirudishe fedha hizo mahali zilipokuwa lakini juhudi hizo
hazikuzaa matunda.
“Hata
hivyo,Veronica alipoona juhudi zake zimegonga mwamba aliita wanaume
wawili ambao majina yao hayajajulikana.Wanaume hao walipomshika Juma
hapo ndipo Veronica alipopata fursa ya kuchukua kipande cha mti na
kumpiga mume wake na kusababisha kifo chake”,alifafanua Kamwela.
Amesema
wanaume hao baada ya kuona Juma amefariki dunia haraka walikimbilia
kusikojulikana Juhudi zaidi zinaendelea ili waweze kukamatwa na
kufikishwa kwenye vyombo vya sheria.Veronica tayari anashikiliwa na
polisi.CHANZO MOBLOG
0 comments:
Post a Comment