Wednesday, 5 February 2014

EL DERBI MADRILEÑO: REAL MADRID YAINYUKA ATLETICO MADRID3-0!

COPA_DEL_REY-FPEL ESTADIO SANTIAGO BERNABEU Usiku huu ni furaha bwelele baada ya Timu yao Real Madrid kuwatandika Wapinzani wao wa Jadi Atletico Madrid Bao 3-0 katika Mechi ya Kwanza ya Nusu Fainali za Kombe la Mfalme, Copa del Rey.
Mechi hii, maarufu huko Jijini Madrid Nchini Spain kama El Derbi madrileño, ilikuwa pia na burudani tosha kwa vitimbwi kati ya Sentahafu wa Real Kepler Laveran Pepe na Fowadi wa Atletico Diego Costa wakifanyiana undava na kutishana huku, kama kawaida yake, Sergio Ramos, akitia chapuo za hapa na pale.
Atletico, ambao ndio Mabingwa Watetezi wa Kombe hili na pia ni Vinara wa La Liga wakiwa Pointi 3 mbele ya Barcelona na Real zinazofungana kwa Pointi, walitinga kwenye Mechi hii wakiwa na nia ya kujihami kwa kumwacha Diego Costa kuwa Straika pekee. 
Real, ambao walitawala, walikuwa shapu na kuonana sana, walipata Bao la kwanza Dakika ya 17 baada ya Shuti la Pepe kumbabatiza Insua na kutinga.
Bao la Pili la Real, lilikuwa safi sana, kufuatia ushirikiano mzuri na Jese Rodriguez kumalizia kwenye Dakika ya 57.
Bao la Tatu ni la Shuti la Angel Di Maria ambalo lilimbabatiza Joao Miranda na kutingisha kamba kwenye Dakika ya 73.
Timu hizi zitarudiana huko Estadio Vicente Calderon hapo Jumanne Februari 11 na ili Atletico waendelee kulitetea Taji lao inabidi waichape Real Bao 4-0.
VIKOSI:
REAL MADRID [Mfumo: 4-3-2]:
-Casillas
-Arbeloa, Pepe, Ramos, Coentrao
-Modric, Alonso, Di Maria
-Jese, Benzema, Ronaldo
Akiba: Illarremendi, Morata, Marcelo, Lopez, Isco, Carvajal, Varane
ATLETICO MADRID [Mfumo: 4-2-3-1]:
-Courtois
-Juanfran, Miranda, Godin, Insua
-Koke, Gabi
-Garcia, Diego, Turan
-Diego Costa
Akiba: Manquillo, Rodriguez, Tiago, Sosa, Alderweireld, Adrian, Aranzubia
REFA: Clos Gómez
Barcelona v Real Sociedad
COPA del REY
NUSU FAINALI
[Saa za Bongo]
Marudiano
Jumanne Februari 11
23:00 Atletico de Madrid v Real Madrid CF [0-3] [Estadio Vicente Calderon]
Jumatano Februari 12
24:00 Real Sociedad v FC Barcelona [Estadio Anoeta]
FAINALI
Aprili 19

Related Posts:

0 comments: