>>WADAU WADAI ADHABU YA CARROLL NI KULINDA KOSA LA REFA WEBB!
Kwa mujibu wa Kanuni za FA, Chama cha Soka England, uamuzi wa Jopo Huru ni wa mwisho na hauwezi kukatiwa Rufaa nyingine.
West Ham inasemekana imeiandikia FA
kutaka ombi lao litolewe jibu ifikapo Ijumaa na pia imesisitiza kuwa
itapeleka suala hilo Mahakamani ikiwa watagomewa kitu ambacho hakijawahi
kutokea England.
Wakisaidiwa na Mwanasheria mahiri huko
Uingereza, QC Lord David Pannick, West Ham walituma Barua hiyo
wakielezea kuhuzunishwa kwao na kesi hiyo ya kumwadhibu Andy Carroll na
kumfungia Mechi 3 bila kujitetea.
Carroll alipewa Kadi hiyo Jumamosi
wakati Timu yake inaichapa Swansea City Bao 2-0 na kuonekana na Refa
Howard Webb kuwa alimpiga kipepsi Beki wa Swansea Chico Flores ingawa
marudio ya tukio hilo yalionyesha Beki huyo hakupigwa bali aliparazwa na
mkono wa Carroll juu ya kichwa waliporuka wote juu.
Kifungo hicho kitamfanya Andy Carroll
azikose Mechi 3 muhimu za West Ham ambao wanapigania kukwepa kuburutwa
kwenye vita ya kushuka Daraja.
Mechi ambazo atazikosa Carroll ni zile
na Aston Villa, huko Villa Park Siku ya Jumamosi, na zile za Nyumbani
Uwanjani Upton Park dhidi ya Norwich na Southampton.
Hata hivyo, FA imekataa kusema lolote kuhusu uamuzi huu wa West Ham.
Lakini Wadau wengi wa Soka huko England wanahisi Carroll ameonewa na ‘mwongo’ Chico Flores ndie aliepaswa kuadhibiwa zaidi.
Miongoni mwa walioibuka na kuiponda FA
kwa uamuzi huu ni Meneja wa zamani Neil Warnock ambae sasa ni Mchambuzi
wa Soka aliedai uamuzi huo wa FA ni kumlinda Refa Howard Webb kwa makosa
yake kwa vile anaiwakilisha England kwenye Kombe la Dunia huko Brazil.
0 comments:
Post a Comment