Timu hizi itarudiana Wiki ijayo huko Estadio Anoeta Nyumbani kwa Real Sociedad.
Barca walipata Bao la kwanza katika Dakika ya 44 baada Sergio Busquets kuufuma Mpira baada ya Kona na kufunga.
Lakini wakati huo huo, Sociedad walipata
pigo baada ya Beki wao Iñigo Martínez kutolewa kwa Kadi Nyekundu
alipomlalamikia Refa kwa wao kunyimwa Penati ya wazi kufuatia Beki wa
Barca, Javier Mascherano, kumwangusha Carlos Vela kwenye Boksi.
Bao la Pili la Barca lilikuwa Dakika ya
60 na la kujifunga wenyewe wakati Cesc Fábregas alimmpeneyezea Alexis
Sánchez ambae Shuti lake lilipiga Posti na Beki Gorka Elustondo
alipojaribu kuokoa Mpira ulimgonga Kipa Eñaut Zubikarai na kutinga
wavuni.
Mapema hiyo Jana, kwenye Nusu Fainali
nyingine huko Santiago Bernabeu, Real Madrid iliwachapa Wapinzani wao wa
Jadi, Atletico Madid, Bao 3-0.
VIKOSI:
BARCELONA [Mfumo 4-3-3]:
-Pinto
-Alves, Pique, Mascherano, Alba
-Xavi, Busquets, Fabregas
-Alexis, Messi, Pedro
Akiba: Adriano, Song, Puyol, Tello, Iniesta, Valdes, Roberto
REAL SOCIEDAD: [Mfumo 5-3-2]:
-Zubikarai
-Martinez, Martinez
-Zaldua, Ansotegi, Angel
-Zurutuza, Gaztanaga, Elustondo
-Griezmann, Vela
Akiba: Canales, Prieto, Bravo, Gonzalez, Pardo, Seferovic, Ros
REFA: González González
COPA del REY
NUSU FAINALI
[Saa za Bongo]
Marudiano
Jumanne Februari 11
23:00 Atletico de Madrid v Real Madrid CF [0-3] [Estadio Vicente Calderon]
Jumatano Februari 12
24:00 Real Sociedad v FC Barcelona [0-2[ [Estadio Anoeta]
FAINALI
Aprili 19
0 comments:
Post a Comment