Waziri wa Viwanda na Biashara, Dk Abdallah Kigoda.
Serikali
imekiri mfumo wa ulipaji kodi na ule wa utumiaji wa mashine za kutolea
risiti(EFDs) kuwa ni mbovu na hivyo unahitaji kufanyiwa kazi.
Waziri
wa Viwanda na Biashara, Dk Abdallah Kigoda, amesema mfumo wa ulipaji
kodi nchini bado unakabiliwa na matatizo ambayo hayawezi kusaidia katika
kumuendeleza mfanyabiashara zaidi ya kumkandamiza.
Dk
Kigoda alisema hayo wakati alipokutana na wafanyabiashara wa mikoa yote
nchini, kuhusu maboresho katika ukusanyaji wa mapato yatokanayo na kodi
na tozo mbalimbali wanazotozwa wafanyabiashara, wajasiriamali na
mapendekezo ya uendeshaji wa biashara nchini.
Alisema
baada ya serikali kulitambua hilo hivi sasa inajipanga kutafuta
ufumbuzi utakaosaidia kumaliza changamoto hizo. Hata hivyo, bado kuna
kazi kubwa ya kupata mfumo bora wa uendeshaji biashara na ulipaji kodi.
“Suala
la mashine za kutolea stakabadhi mmelizungumzia kwa mapana, lakini hata
hivyo bado zina changamoto lakini haya yote mliyoyazungumza wakati
nikienda kukutana na wenzangu endeleeni na kufanya biashara zenu kwa
utaratibu wenu wa zamani hadi ufumbuzi utakapatikana,” alisema Dk
Kigoda.
Dk
Kigoda alisema kama mtakumbuka kuna taarifa zilizowahi kutolewa na
vyombo vya habari kimataifa kuwa Tanzania ilikuwa ni moja ya nchi
iliyofanya vibaya katika kipindi cha mwaka jana kutokana mfumo mbaya
uliosbabishwa na sababu mbalimbali ikiwamo masuala ya ukusanyaji kodi.
Aidha,
aliwataka kuwa wavumilivu wakati matatizo yao yakishughulikiwa kwani
watambue matatizo ya kiuchumi hayatatuliwi kwa migomo, maandamano ya
kisiasa bali hutatuliwa kiuchumi.
“Tanzania
tuna tatizo kubwa sana na lazima tuliondoe hili siyo lingine bali ni
kutoaminiana kati ya serikali na wafanyabiashara. Hili lazima tulitatue
kwa sababu serikali tunaona wafanyabiashara ni wajanja wanaweza kukwepa
kodi wakati wafanyabiashara nao hivyo hivyo….” alisema na kuongeza:
Huku
akishindwa kuweka wazi akiepuka kulizungumzia kwa undani suala la EFD,
zaidi akiwapongeza wafanyabiashara hao kwa kauli yao kuwa hawapingi
kulipa ko.iN Aliwasihi suala hilo litakwisha baada ya kikosi kazi
kitakachoundwa kikiwashirikisha wafanyabiashara hao.
“Hatuwezi
kumkamua ng’ombe atoe maziwa bila kumpa majani na hatuwezi kumaliza
matatizo ya uchumi kwa maandamano au kuwasikiliza wanasiasa. Njia pekee
ya kutatua matatizo haya ni kushirikisha wataalamu wa uchumi” aliongeza.
Dk
Kigoda alisema waraka uliotolewa na wafanyabiashara utafanyiwa kazi na
haki itatolewa baina ya mfanyabiashara mkubwa, wa kati na mfanyabiashara
mdogo
Alisema
serikali itaunda kikosi kazi kitakachoshirikisha jumuiya hiyo ya
wafanyabiashara ili waweze kuwekeza katika mazingira mazuri.
Dk
Kigoda alisema kupitia utaratibu huo ni vyema wakaangalia mfumo wa
ulipaji kodi uwe ni mfumo unaoendeleza biashara na sio mfumo unaotoa
kodi ili zitumike.
“Kupitia
utaratibu huu ni vyema tukaangalia mfumo wa ulipaji kodi uwe ni mfumo
wa kuendeleza kodi na sio kulipa kodi ili tutumie na kwamba hapa tutakaa
kikao na wenzangu na wa TRA na Wizara ya Fedha na baada ya hapo tutatoa
tamko”alisema Dk Kigoda na kuongeza
“Nawahakikishia
mimi kama waziri mwenye dhamana ya viwanda na biashara lengo langu
kubwa ni kusukuma serikali katika punguza gharama za biashara kwa
wafanyabiashara na changamoto yetu hii ya utumiaji wa mashine hizi
tutamaliza kupitia taratibu za kiuchumi”alisema
Katika
hatua nyingine, Waziri Kigoda amewatetea wafanyabiashara wadogo
manaofanya baishara zao katika maduka ya Kariakoo kwa kusema kuwa
wanachangia pato la taifa katika kukuza uchumi.
“Wafanyabaishara
wadogo ndio wanaochangia pato la taifa katika kukuza uchumi wa nchi
tofauti na wafanyabaishara hao wakubwa na hata hivyo wafanyabaishara hao
wakubwa walianzia kama hao wafanyabiashara wadogo”aliongeza.
Pia
amewakalipia askari wanaofanya doria katika soko la Karikaoo maarufu
kama “Tigo” kutoka na wafanyabaishara hao kudai kuwa askari hao wamekuwa
tishio kwa kuwakamata bila kufauata utaratibu.
Mwakilishi kutoka Zanzibar
Mwakilishi
kutoka Zanzibar Lacky Zahoor alisema tatizo kubwa ni ulipaji wa kodi
katika nchi hiyo kwamba huko Zanzibar mashine hizo hwazihitaji kwa
sababu zina tunza kumbukumbu zao sio hasara zao.
“Sisi
tupo tayari kulipa kodi lakini mfumo uboreshwe uwe mzuri kwa ni hizi
mashine kwetu Zanzibar hatuzitaki kwa sababu hazionyeshi hasara
tunayopata sisi zaidi ya kumbukumbu zao tu hivyo hatuzikubali”alisema
Zahoorn
Mshauri wa Jumuiya wafanyabiashara wa Kariakoo.
Mshauri
wa Jumuiya wafanyabiashara wa Kariakoo, Johnson Minja alisema chimbuko
linaloonekana kuwa mzigo kwa wafanyabiashara hao ni kitendo cha Mamlaka
ya Mapato Tanzania (TRA), kuingia katika awamu ya pili ya utumiaji wa
mashine hizo za kukusanyia kodi, bila kufanya tathimini ya kutosha juu
mafanikio na changamoto zilizojitokeza wakati wa awamu ya kwanza ya
utumiaji mashine hizo.
Chanzo: Mwananchi
0 comments:
Post a Comment