. Ni siku moja baada ya Rais Bashir al Assad kuanza kukabidhi silaha za kemikali
.watoto wadogo chini ya miaka 8 ni miongoni kwa waliookolewa kwenye mji wa Damascus
.mashambulizi hayo ya ndege yalifanywa na vikosi vya serikali vya Bashar Assad, wanasema wanaharakati
.silaha za kemikali zilibebwa kwenye meli ya Denmark chini ya ulinzi mkali wa majeshi ya Umoja wa Mataifa
Na Damas Makangale, MOblog kwa Msaada wa Mtandao
Mtoto
mchanga wa miezi kadhaa amenasuliwa kutoka katika mabaki ya nyumba
baada ya mashambulizi makali ya majeshi ya anga na vikosi vya serikali
vya Rais Bashir al Assad juzi na kufunikwa na blanketi kutokana na hali
ya hewa kuwa mbaya nchi humo.
Taarifa
zinasema idadi kubwa ya watu wasio kuwa na hatia wanahofiwa kupoteza
maisha katika mashambulizi hayo ya ndege za kivita kutoka kwa askari
watiifu wa Rais Assad mjini Damascus.
Mashahidi
waliona mashambulizi hayo wanasema waliona helikopta za kijeshi
zikimwaga mabomu makubwa na vumbi kubwa kutimka kati kati ya makazi ya
raia wasio na hatia katika wilaya ya Douma nje kidogo wa mji mkuu
Damascus.
Wanaume
na vijana walikuwa katika harakati za kuwatoa watoto wadogo kwenye
vifusi baada ya shambulio kubwa kupata kutokea tangu mgogoro wa Syria
uanze miaka mitatu iliyopita.
Wanaharakati
wanasema shambulio hilo lilifanywa na vikosi vinavyomuunga mkono Rais
Bashar Assad, baada ya baraza la usalama wa Umoja wa Mataifa kusisitiza
kwamba Serikali ya Damascus kukabidhi silaha za kemikali na sumu.
Hiyo
imekuja baada ya uthibitisho kwamba Serikali ya Damascus inatumia
kemikali katika kuwadhibiti waasi wan chi hiyo na katika kitongoji cha
Ghouta Agosti 21 mwaka jana vikosi vya serikali kuua mamia ya watu kwa
kutumia kemikali na sumu kali.
0 comments:
Post a Comment