Na DIANA BISANGAO, Matukiodaima.com Iringa
Watu wawili wafariki dunia mkoani Iringa katika matukio
mawili tofauti likiwemo la mwanaume mmoja mkazi wa kijiji cha Nyamihuu mkoani
Iringa kupata ajali ya trekta aliyokuwa akiendesha kuacha barabara na
kupinduka.
Imedaiwa mwanaume huyo aliyetambulika kwa jina Herman Sanga
(22) alikuwa akiendesha trekta lenye namba za usajili 6656 aina ya Fiat mali ya
Kriakos Kalogeresi mkazi wa Iringa alikuwa akitokea shambani akielekea nyumbani
ambapo trekta alilokuwa akiendesha liliacha barabara na kupinduka na kusababisha majeruhi.
Akizungumza na wandishi wahabari ofisini kwake
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Iringa Ramadhani Mungi alithibitisha kutokea kwa
tukio hilo lililotokea January 5.
Hata hivyo alisema kuwa majeruhi huyo alikimbizwa katika
hospitali ya serikali Tosamaganga kwa matibabu zaidi ambapo majira ya saa mbili
usiku alifariki dunia akiwa anapatiwa matibabu, Kamanda Mungi alisema chanzo
cha ajali hiyo ni mwendo kasi.
Wakati huohuo Jeshi la polisi Mkoani Iringa linamshikiria
mtuhumiwa mmoja aliyejulikana kwa jina la Denis Kamugisha (34) kwa kosa la kumgonga mwendesha pikipiki
ambaye jina lake halijafahamika na kusababisha kifo kwa abiria wake aitwaye
Costantine Msuva mkazi wa boma la ng’ombe huku dereva wa pikipiki akiwa
amelazwa na hawezi kuzungumza.
Kamanda Mungi alisema kuwa tukio hilo lilitokea mnamo tarehe
5 january majira ya saa 9:50 alasiri maeneo ya Boma la Ng’ombe Kata ya Kidabaga
Tarafa ya Kilolo Wilaya ya Kilolo ambapo mtuhumiwa huyo alikuwa akiendesha gari
aina ya land cruser lenye namba za usajiri T.222 APR alimgonga mwendesha
pikipiki aina ya sky mark ambapo namba za usajiri hazijafahamika, chanzo cha
ajali bado hakijafahamika.
Aidha Kamanda Mungi amesema mbali na matukio hayo mawili ya
ajali tofautitofauti pia watu wasiofahamika waliiba ng’ombe kumi na tisa (19)
wenye thamani ya shilingi milioni kumi na moja za kitanzania (11000000/=Tshs)
mali ya Maganga Madagana (27) mkazi wa kijiji cha Mfyome, chanzo cha tukio hilo
kinaeleza ni tama ya mali ambapo watuhumiwa wanatafutwa.
0 comments:
Post a Comment