Monday, 12 October 2015

KAMANDA MPINGA AKABIDHI TBL,RIPOTI YA UPIMAJI AFYA ZA MADEREVA

 
 KAMANDA wa Polisi Kikosi cha Usalama Barabarani Nchini, Kamishna Mohamed Mpinga (katikati), akikabidhi Ripoti ya upimaji wa Afya za Madereva kwa Meneja Mahusiano ya Nje wa Kampuni ya Bia Tanzania (TBL), Bi. Emma Oriyo, Dar es Salaam jana, baada ya zoezi la kupima Afya za madereva lililofanyika Mikese, mkoani Morogoro, Msata mkoani Pwani na Segera, mkoani Tanga. Kushoto ni Kamanda wa Kikosi cha Afya cha Jeshi la Polisi, Kamishna Msaidizi, Paul Kasabago.
 KAMANDA wa Polisi Kikosi cha Usalama Barabarani Nchini, Kamishna Mohamed Mpinga (katikati), akizungumza na waandishi wa habari, Dar es Salaam jana, baada ya kukabidhi Ripoti ya Upimaji wa Afya za Madereva kwa Meneja Mahusiano ya Nje wa Kampuni ya Bia Tanzania (TBL), Bi. Emma Oriyo. (Kushoto ni Kamanda wa Kikosi cha Afya cha Jeshi la Polisi, Kamishna Msaidizi, Paul Kasabago.
 Meneja Mahusiano ya Nje wa Kampuni ya Bia Tanzania (TBL), Bi. Emma Oriyo, akizungumza na waandishi wa habari, Dar es Salaam jana baada ya kupokea Ripoti ya Upimaji wa Afya za Madereva kutoka kwa Kamanda wa Polisi Kikosi cha Usalama Barabarani, Kamishna Mohamed Mpinga (katikati), ambaye pia aliipokea kwa Mkuu wa Kikosi cha Afya cha jeshi hilo, Kamishna Msaidizi Paul Kasadago (kushoto).
KAMANDA wa Polisi Kikosi cha Usalama Barabarani Nchini, Kamishna Mohamed Mpinga (katikati), akionyesha Ripoti ya upimaji Afya za MAdereva, baada ya kuipokea kutoka kwa Kamanda wa Kikosi cha Afya cha Jeshi la Polisi, Kamishna Msaidizi Paul Kasabago, Dar es Salaam jana. Kulia ni Meneja Mahusiano ya Nje wa Kampuni ya Bia Tanzania (TBL). 

0 comments: