Sunday, 26 January 2014

JUAN MATA: MAHOJIANO YA KWANZA KAMA MCHEZAJI MAN UNITED!

>>MATA: “DE GEA ALIKUWA AKINITUMIA SMS: “LINI UNAKUJA, LINI UNATUA, UNAKUJA NA HELIKOPTA AU BAISKELI?”
MATA-ASAINI_MKTABAJUAN MATA, Mchezaji mpya wa Mabingwa wa England Manchester United, ambae alisainiwa kwa Dau kubwa ambalo ni Rekodi kwa Klabu hiyo, amefanya Mahojiano yake ya kwanza na MUTV, Kituo cha TV cha Mabingwa hao.
YAFUATAYO NI MAHOJIANO YOTE:
MWAHAHABARI: UNAJISKIAJE HATIMAE KUWA MCHEZAJI WA MAN UNITED?
JUAN MATA: Ni Siku ya furaha kubwa kwangu, kukutana na Wachezaji wenzangu, Meneja, kuona Uwanja wa Mazoezi. Hii ni Klabu kubwa mno na nasikia fahari kuwa hapa.
ULIPITIWA NA FIKRA GANI ULIPOSIKIA MAN UNITED INAKUTAKA?
Nilihisi mshangao! Hii ni Timu iliyoshinda Ubingwa mara nyingi katika Historia ya Ligi Kuu na Ligi ya England. Inashangaza Klabu kama hii kuwa na nia na wewe. Nilijisikia vizuri sana.
WACHEZAJI WENGI WAMETUA HAPA LAKINI WEWE NDIO MWENYE REKODI, JE HUJISIKII PRESHA?
Najua ni Dau kubwa lakini nina imani kila kitu kitakuwa sawa. Nitajaribu kadri ya uwezo wangu kama Siku zote ninavyofanya. Kikosi na Meneja wote ni wazuri na Mashabiki ni wazuri mno -tuna kila kitu cha kupata mafanikio.
ULIKUWA NA WAKATI MZURI CHELSEA NA MCHEZAJI BORA KWA MISIMU MIWILI, JE HUSHANGAZWI KUWA HAPA HASA KWA VILE KLABU KUBWA HAZIUZI WACHEZAJI WAO KWA WAPINZANI?
Ukweli, inashangaza. Lakini lazima niseme naishukuru Chelsea, kwa Mmiliki, kila Mtu anaefanya Klabuni na Mashabiki ambao walinichagua Mchezaji Bora kwa Misimu miwili na Siku zote nitawashukuru. Wamekuwa ajabu kwangu. Miezi 6 iliyopita ilikuwa migumu kwangu kwa vile sikucheza mara nyingi kama nilivyotaka. Najua hii ni Gemu ya Kitimu na naheshimu hilo. Lakini kupata nafasi kuja Manchester United ni kitu kikubwa mno kwangu ili kujiendeleza katika maisha yangu ya Soka kwenye hii Klabu kubwa mno.
DAVID DE GEA ALIKUWA AKIKUNGOJEA UFIKE, AMEKWAMBIA NINI KUHUSU MAISHA HAPA?
Amekuwa akinitumia Ujumbe wa Simu mara kwa mara Siku za hivi karibuni akisema: “Lini unakuja, Lini unatua, Unakuja na Helikopta au Baiskeli?” Nipo hapa sasa na nimefurahi sana kuwa hapa na hasa kuwa na David. Yeye ni Rafiki yangu, Kipa mzuri na Mtu mwema sana. Yeye alikuwa muhimu kuja kwangu hapa!
UNAJISIKIAJE NA NAFASI YA KUCHEZA PAMOJA NA KINA WAYNE ROONEY, ROBIN VAN PERSIE NA ADNAN JANUZAJ KWA KUWATAJA WACHACHE?
Ni wazi kwa Mchezaji kama mimi ambae hujaribu kufunga, kutoa msaada wa kufunga na kujaribu kuwa mbunifu ni kitu bora kucheza na Wachezaji wa aina hii.
Wayne Rooney, Robin van Persie, Adnan, Valencia, Chicharito, Welbeck... wote ni Wachezaji wa kiwango cha juu na nitajaribu kufanya vyema kwa ajili ya Timu.
UNAFIKIRI IPI NI POZISHENI YAKO BORA?
Kwanza ni kucheza! [Huku akicheka]. Napenda kucheza. Nadhani naweza kucheza katika nafasi tatu nyuma ya Straika. Nilipofika Chelsea nilicheza kushoto, Msimu huu nimecheza kulia na Msimu uliopita, ambao ulikuwa Msimu wangu bora, nilicheza nyuma tu ya Straika.. Lakini hilo sijali mradi nacheza.
UMETWAA MATAJI MENGI KATIKA MAISHA YAKO LAKINI HAPA UNATAKA MAFANIKO GANI?
Ningependa kutwaa Ubingwa wa Ligi Kuu. Ni Kombe Spesho kwa kila Mchezaji anaecheza Nchi hii. Kwenye Klabu hii naamini unaweza kushinda chochote. Nitajaribu kadri ya uwezo wangu. Mie bado Kijana na nimebahatika kutwaa Vikombe lakini nataka kutwa vingine zaidi.
MENEJA AMESEMA ANA NIA KUKUONA WEWE UKICHEZA GEMU YA JUMANNE NA CARDIFF, JE UTAJISKIAJE KUTINGA UWANJANI OLD TRAFFORD KAMA MCHEZAJI WA MAN UNITED?
Old Trafford ni Uwanja mkubwa na wa kushangaza kucheza Soka ndani yake. Nimeshakuwa hapa mara mbili au tatu na Siku zote na Wapinzani na sasa nina nafasi kucheza kama Nyumbani. Itakuwa ni tofauti lakini najua itakuwa ni kitu kikubwa mno hasa kwa vile Mashabiki hapa ni bora mno.

0 comments: