Kamanda wa Polisi mkoa wa Singida,SACP Geofrey Kamwela.
Na Nathaniel Limu, Singida
DIWANI
wa kata ya Umyambwa tarafa ya Mungumaji Halmashauri ya Manispaa ya
Singida,(CCM) Shaban Satu na watu wengine tisa,wanashikiliwa na jeshi la
polisi kwa tuhuma ya kuchoma moto basi la kampuni ya Mtei Express ya
mjini Arusha.
Diwani
huo na wapiga kura wake,inadaiwa kulichoma moto basi hilo januari tisa
mwaka huu saa moja na dakika moja barabara ya Singida-Arusha eneo la
kijiji cha Kisasida manispaa ya Singida.
Watuhumiwa
hao walifikia uamuzi huo kutokana na basi hilo T.742 ACU lililokuwa
linaendeshwa na Dismas Ludovick, kugonga bodaboda T.368 BXZ iliyokuwa
imepakia watu wanne wa familia moja.
Wanafamilia
hao ambao walikuwa wakienda shamba,ni Tamili,Kassim na Hamza ambao ni
watoto wa Shabani Bunku ambaye alikuwa akiendesha bodaboda hiyo.Watoto
wote watatu walipoteza maisha na baba yao bado anaendelea na matibabu
katika hospitali ya misioni ya Hydom mkoani Manyara.
Kamanda
wa polisi mkoa wa Singida,SACP Geofrey Kamwela,amekiri dwani huyo na
wapiga kura wake kukamatwa kwa tuhuma ya kuchoma moto basi la
Mtei.Ameahidi kutoa taarifa zaidi kazi itakapomalizika.
Mwandishi
wa habari hizi alishuhudia watuhumiwa hao wakishushwa kutoka gari la
polisi kwenye kituo cha kati cha polisi mjini hapa.
0 comments:
Post a Comment