KWA MARA nyingine tena, Etihad ilishuhudia mvua ya Magoli wakati Jana Usiku Manchester City ilipoifumua
West Ham Bao 6-0 katika Mechi ya Kwanza ya Nusu Fainali ya Capital One Cup.
Timu hizi zitarudiana huko Upton Park hapo Januari 21.
Hiki ni kipigo cha pili kikubwa kwa West
Ham baada Wikiendi iliyopita kutandikwa Bao 5-0 na Nottingham Forest na
kutupwa nje ya FA CUP.
CAPITAL ONE CUP
RATIBA/MATOKEO:
NUSU FAINALI
Jumanne Januari 7
Sunderland 2 Man United 1
Jumatano Januari 8
Man City 6 West Ham 0
Marudiano
[Saa 4 Dakika 45 Usiku]
Jumanne Januari 21
West Ham v Man City
Jumatano Januari 22
Man United v Sunderland
Hadi Mapumziko Man City walikuwa mbele kwa Bao 3-0 kwa Bao mbili za Alvaro Negredo na Yaya Toure.
Kipindi cha Pili, Man City waliongeza Bao nyingine 3 huku Negredo akikamilisha Hetitriki yakena Edin Dzeko kupiga Bao 2.
Juzi, katika Mechi nyingine ya Nusu
Fainali, Sunderland waliifunga Man United Bo 2-1 na Timu hizi
zitarudiana huko Old Trafford hapo Januari 22.
VIKOSI:
Man City: Pantilimon; Zabaltea, Kompany, Lescott, CLichy; Nasri, Touré, Garcia, Silva; Negredo, Dzeko
Akiba: Hart, Milner, Kolarov, Fernandinho, Demichelis, Nastasic, Lopes
West ham: Adrian; Demel, Johnson, O'Brien, McCartney, Taylor; J Cole, Noble, Diamé, Downing; Maiga
Akiba: Jarvis, Rat, Collison, Diarra, C Cole, Morrison, Jaaskelainen
Refa: J Moss
0 comments:
Post a Comment