>>NUSU FAINALI NI BONGO v UGANDA!!
Mapinduzi Cup, Kombe la Kusheherekea Miaka 50 ya Mapinduzi ya Zanzibar, Usiku huu limemaliza Mechi zake
za
Robo Fainali na Mechi za Nusu Fainali zitashindaniwa na Timu toka
Uganda dhidi ya Timu kutoka Tanzania Bara katika Mechi zote mbili.
Mabigwa Watetezi, Azam FC, wao walitinga
Nusu Fainali kwa kuichapa Clove Stars, Kombaini ya Pemba, Bao 2-0, URA
ya Uganda kuitungua KMKM 1-0, Tusker ya Kenya na KCC ya Uganda kutoka
0-0 katika Dakika 90 na KCC kuibuka Mshindi kwa Mikwaju ya Penati.
Simba, wakicheza Mechi ya mwisho ya Robo
Fainali Uwanjani Amaan Saa mbili Usiku huu waliichapa Chuoni ya
Zanzibar Bao 2-0, Bao zote zikifungwa na Ramadhan Singano.
RATIBA/MATOKEO:
ROBO FAINALI
Jumatano Januari 8
Gombani Stadium, Pemba
KMKM 0 URA 1
Azam FC 2 Clove Stars 0
Amaan Stadium
Tusker 0 KCC 0 [KCC imesonga kwa Penati 4-3]
Simba 2 Chuoni 0
NUSU FAINALI
Ijumaa Januari 10
SAA 10 JIONI: Azam FC v KCC
SAA 2 USIKU: URA v Simba
Nusu Fainali, ambazo zitachezwa Ijuma Januari 10, Azam FC itaivaa KCC na Simba kupambana na URA.
Fainali ni Jumatatu Januari 13 kwenye Uwanja wa Amaan Jijini Zanzibar.
0 comments:
Post a Comment