>>MAN UNITED NJE KWA MATUTA!!
MSIMU
wa balaa kwa Mabingwa wa England Manchester United umeendelea tena
baada kutupwa nje ya Capital One Cup kwa Mikwaju ya Penati na Sunderland
Usiku huu Uwanjani Old Trafford.
Wakiwa nyuma kwa Bao 2-1 baada kufungwa
Mechi ya Kwanza huko Stadium of Light, Man United walikuwa wakiongoza
Bao 1-0, kwa Bao la Jony Evans, hadi mwisho wa Dakika 90 na hivyo
kufungana Bao 2-2 na Sunderland, na Mechi hi kulazimika kwenda Dakika za
Nyongeza 30 kwa vile Goli za Ugenini zinahesabiwa tu baada ya Dakika
120.
Lakini, kwenye Dakika ya 119, Phil
Bardsley, aliisawazishia Sunderland na licha ya Man United kushinda
Mechi hii Bao 2-1 baada Chicharito kufunga Bao katika Dakika ya 120, na
kufanya Jumla ya Magoli iwe 3-3, ilibidi Mshindi aamuliwe kwa Penati.
Sunderland walishinda kwa Jumla ya Penati 2-1.
Kwenye Fainali, Sunderland watacheza na Man City hapo Machi 2.
VIKOSI VINAVYOANZA:
MANCHESTER UNITED: De Gea; Rafael, Smalling, Evans, Buttner; Januzaj, Carrick, Fletcher, Kagawa; Welbeck, Hernandez.
Akiba: Evra, Jones, Giggs, Lindegaard, Young, Cleverley, Valencia.
SUNDERLAND: Mannone, Bardsley, Alonso, Brown, O'Shea (c), Cattermole, Colback, Ki, Johnson, Borini, Fletcher.
Akiba: Ustari, Vergini, Larsson, Gardner, Celustka, Altidore, Giaccherini.
REFA: Lee Mason
CAPITAL ONE CUP
RATIBA/MATOKEO:
NUSU FAINALI
Jumanne Januari 7
Sunderland 2 Man United 1
Jumatano Januari 8
Man City 6 West Ham 0
Marudiano
[Saa 4 Dakika 45 Usiku]
Jumanne Januari 21
West Ham 0 Man City 3 [Jumla bao 0-9]
Jumatano Januari 22
Man United 2 Sunderland 1[Jumla bao 3-3, Sunderland Washindi Penati 2-1]
FAINALI
Jumapili Machi 2
Wembley Stadium London
Man City v Sunderland
0 comments:
Post a Comment