Thursday, 17 October 2013

ZITTO ASIMAMA KIDETE JUU YA UKAGUZI WA HESABU ZA VYAMA

Picture MWENYEKITI wa Kamati ya Hesabu za Serikali (PAC), Kabwe Zitto, ameendelea kusisitiza kuwa hadi sasa hakuna chama chochote cha siasa kilichowasilisha ripoti ya ukaguzi wa hesabu zake kwa Msajili wa Vyama vya Siasa na kuvitaka vyama hivyo kuacha propaganda na kulichukulia suala hilo kisiasa.

Amesema hazungumzi suala hilo kama Naibu Katibu Mkuu wa CHADEMA, bali anasimamia Sheria na kama hawataki, wamshauri Spika wa Bunge, Anne Makinda, avunje kamati yake.

“Napenda niwaambie nazungumzia suala hili si kama Naibu Katibu Mkuu wa CHADEMA bali Mwenyekiti wa PAC na ninasimamia sheria,” alisema.

Akizungumza jana katika ofisi ndogo za Bunge jijini Dar es Salaam, Zitto alisema tangu atoe tamko la kutaka vyama hivyo vijiandae kujieleza kwanini havijawasilisha ripoti hizo za ukaguzi, amekuwa akisikia kelele tu na hakuna chama chochote kilichotekeleza

 

 
Ifuatayo, imenukuliwa kutoka kwenye gazeti la HabariLeo 

0 comments: