Makamu wa Rais,Dk. Mohammed Gharib Bilal na
Mwenyekiti wa Chama cha Wamiliki wa Vyombo vya Habari nchini (Moat),
ambaye pia ni Mwenyekiti Mtendaji wa IPP, Dk. Reginald Mengi (kushoto),
wakitoa heshima za mwisho mbele ya mwili wa marehemu Julius Nyaisanga,
aliyekuwa mtangazaji mkongwe wa redio hapa nchini. Shughuli za kuuaga
mwili wake ilifanyika katika viwanja vya Leaders Kinondoni jijini Dar es
Salaam jana na mwili wake ulitarajiwa kusafirishwa kwenda Wilaya ya
Tarime mkoani Mara kwa maziko.
Wanahabari jijini Dar es Salaam na wadau wengine jana waliuaga mwili wa aliyekuwa mtangazaji mkongwe nchini, Julius Nyaisanga maarufu kama ‘Uncle J’ (53), ayefariki dunia mwishoni mwa wiki iliyopita mkoani Morogoro.
Mamia ya wanahabari hao na wadau wengine wakiongozwa na Makamu wa Rais, Dk. Mohammed Gharib Bilal, walitoa heshima zao za mwisho katika viwanja wa Leaders Club jijini Dar es Salaam.
Mwili wa marehemu Nyaisanga ulipokelewa na wanahabari na wadau wengine waliokuwapo kabla ya kufanyika ibada fupi ya kumuombea na baadaye uliagwa rasmi.
0 comments:
Post a Comment